Askari wa Kikosi cha Zimamoto Zanzibar wakiwa takita zoai la kuuzima moto wakati nyumba moja katika Mji Mkongwe wa Zanzibar ikiwaka moto.
Kikosi cha Jeshi la Zimamoto wamefanikiwa kuudhiniti moto huo na kufanikiwa kuuziwa kunusuru majengo mengi karibu na jengo hilo na kupata changamoto nyingi kutokana hali ya mazingira ya eneo hilo.
Mwanchi aliyefariki ni mkaazi wa nyumba hiyo Bi. Rehema Chande alijaribu kujiokoa kwa kuruka nje akiwa na mtoto wake na kumkuta mauti na Mtoto wake Nabil Issa amepata majaraha na kukimbizwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kupata huduma ya kwanza, kwa mujibu wa Wananchi walioshuhudia tukio hilo.
Wananchi wakifuatilia zoezi la uzimaji wa moto katika nyumba moja iliyoko katika mtaa wa mji mkongwe Kiponda Wilaya ya Mjini Unguja ikiwaka moto, katika zoezi hilo kikosi cha Zimamoto Zanzibar wamefanikiwa kuuzima moto huo leo 30-8-2022.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto Zanzibar wakiendelea na zoezi la uzimaji wa moto katika nyumba moja iliyopata ajali hiyo katika mtaa wa Kiponda Mji Mkongwe wa Unguja Jijini Zanzibar leo 30-8-2022.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa akipata maelezo kutoka kwa Sheha wa Kiponda alipofika katika eneo la jali hiyo katika mtaa wa kiponda leo kutembelea na kuwafariji Wananchi waliopata maafa hayo ya kuunguliwa na kupata msiba wa ndugu yao Marehemu Rehema Chande, kutokana na ajali hiyo ya moto iliyotokea leo majira ya asubuhi.
Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mhe. Mahmoud Mussa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe. Rashid Msaraka wakitembelea eneo la ajali ya moto mtaa wa kiponda na kuwafariji wananchi waliopata mafaa hayo leo.
KAMISHNA wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar Rashid Mzee Abdalla akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar baada ya kukamilika kwa zoezi la uzimaji wa moto katika mtaa wa Kiponda Mji Mkongwe Jijini Zanzibar, Kikosi chake kimefanikiwa kuudhibiti moto huo kutoleta madhara kwa majengo ya jirani na nyumba hiyo iliyopata ajali ya moto.
kulikuwa na changamoto za hapa na pale kutokana na mazingira ya mitaa hiyo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment