Habari za Punde

Wasanii Kutoka Nchini Tanzania Watashiriki Maonesho ya "nternational Afrika Expo Festival "Maarufu Kama "Umoja wa Afrika " Yanayotarajiwa Kufanyika 01 September hadi 04 September 2022 Mjini Tuebingen Ujerumani

Na.Zainabu Ally Hamisi - Tuebingen.Germany.                                                                      
Yale Maonyesho makubwa nchini Ujerumani  "International Afrika Epo Festival pia maarufu kama "UMOJA WA AFRIKA" International Festival.yanatarajiwa kuanza wiki siku Alhamisi September 1 hadi 4 September 2022 katika viwanja vya Fest Platz mjini Tuebingen ,nchini Ujerumani,ambako watanzania wengi wakiwamo wasanii wameshatua ujerumani kushiriki katika maonyesho hayo..

Miongoni mwa wasanii hao ni wachoraji na wa bunifu wa picha 'Visual Arts"
mchoraji Bw.Chilonga Hajji na mwenzake Meddy kutoka Tanzania,pia yupo mwanamitindo na rafiki wa mazingira Diana Magesa akiwa na mwenzie Bi.Rabiah  Al-Karitty kutoka Tanzania ambao wanamitindo hawa wamewahi kushiri maonyesho mengi ya kimataifa yakiwemo New 

York Fashion week,Unesco Paris,Ufaransa,Toronto Fashion week,Canada. vikundi vya sanaa za maonyesho na bendi za muziki nazo zipo tayari kunogensha maonyesho hayo makubwa ,bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Band" aka FFU inayoongozwa na mwanamuziki kamanda Ras Makunja na muziki wao wa dansi nao watakuwepo. mwanamuziki wa mtindo wa Reggae kutoka Tanzania Saidon na The Train Band ambao wana maskani yao ujerumani nao watatumbuiza, ALI BAYO TRADITION Group (Senegal), kikundi cha Cameroon Balet navyo vitakuwepo na wasanii wengi wengi tu. mwandishi wa habari Zainabu Ally Hamisi anaripoti kutoka Tubingen.Ujerumani.https://www.africafestival-international.org

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.