Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameshiriki Maziko ya Askofu Mstafu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar Marehemu John Ramadhan

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar kuhudhuria maziko ya Marehemu Askofu Mstafu wa Kanisa la  Anglikana  Zanzibar John Ramadhan, yaliyofanyika leo 17-9-2022, katika viwanja vya kanisa hilo Mkunazini Wilaya ya Mjini Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihudhuria maziko ya Marehemu Askofu Mstafu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar John Ramadhan, yaliofanyika katika Kanisa la Mkunazini leo 17-9-2022 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu Mhe. Georg Mkuchika na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Shaban


Mwanafamilia wa Marehemu Askofu Mstafu John Ramadhan akisoma wasifu wa marehemu baada ya kumalizika kwa Ibada ya kumuombea iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana Mkunazini Jijini Zanzibar leo 17-9-2022 wakati wa maziko yake yaliyofanyika katika viwanja vya Kanisa hilo. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Askofu Mstafu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar leo 17-9-2022. Maziko yaliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la Anglikana Mkunazini Wilaya ya Mjini Unguja leo


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Askofu Mstafu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar John Ramadhan, maziko hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la Mkunazini Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 17-9-2022

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.