Na Khadija Khamis – Maelezo.
Ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi umekua ukiongezeka kwa kasi siku hadi siku na kupelekea kuwaathiri wanawake wengi hapa nchini.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari juu ya elimu ya kinga ya Saratani ya Shingo ya kizazi kwa wanawake, Mratibu wa Kitengo cha Maradhi Yasioambukiza kutoka Hospitali ya Rufaa Mnazi mmoja Omar Abdalla Ali amesema maradhi haya yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa hapa nchini.
Amesema shingo ya kizazi inazuilika au kutibika endapo itagundulikana mapema ikiwa kwenye hatua za awali hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara pamoja na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya
wanawake wote walio na umri wa miaka 30 na kuendelea wanatakiwa kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi japo kwa mwaka mara moja
Mratibu huyo amewataka wanawake kuacha kutumia kemikali za aina yoyote kuweka katika sehemu ya uke jambo ambalo huathiri njia ya kizazi na kupeleka kupata saratani ya shingo ya kizazi.
Nae Meneja wa Muungano wa Watu Wanaoishi na Maradhi Yasioambukiza Zanzibar (NCDs) Haji Khamis Fundi ameitaka jamii hasa wanawake kufanya uchunguzi na kuachana na vichecheo vinavyosababisha maradhi hayo.
c
Aidha alisema kukosa elimu ya kujiepusha na Saratani kwa jamii kunachangia kuwepo na kesi nyingi za ugonjwa huwo hivyo aliishauri jamii kujiepusha na vichocheo vya maradhi hayo
Hata hivyo aliitaka jamii kuacha matumizi ya vyakula vyenye kemikali nyingi na vile vya makopo vilivyopita muda wake, matumizi ya tumbaku, sigara, pombe na utiaji wa vitu visivyofaa sehemu za siri pamoja na matumizi ya mionzi ya mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment