Habari za Punde

Wananchi wa Kijiji cha Isupilo Wamkataa Mwekezaji Overland

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kijiji cha Isupilo namna kutatua changamoto na mgogoro huo wa Ardhi.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Isupilo wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakati wa kutafuta njia ya kutatua mgogoro wa ardhi katika kijiji hicho

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Wananchi wa Kijiji cha Isupilo wilaya ya Iringa wamesema kuwa viongozi wa Kijiji hicho wamekuwa chanzo cha migogoro ya ardhi baina ya wananchi na wawekezaji.

 

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo walisema kuwa kumekuwa na mgogoro ambao umedumu miaka mingi.

 

Walisema kuwa kutokana na kutokuwa na uongozi imara kumesababisha familia ya Mzee Kivike kuuza ardhi ambayo imekuwa inakariwa na kufanyika kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na wananchi kwa zaidi ya miaka kumi na tano.

 

Waliongeza kuwa mwekezaji Overland aliponunua shamba kwenye familia ya Mzee Kivike amejiongezea eneo la mipaka la hekari zaidi ya 250 ambayo kwa sasa ndio ambalo linaleta mgogoro na wananchi.

 

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa atamwita mwekezaji Overland, viongozi wa ardhi na viongozi wa Kijiji ili kuhakikisha wanatatua mgogoro huo.

 

Moyo alisema kuwa mgogoro huo wa ardhi utatuliwa kwa njia ya amani kwa kuhakikisha kila mtu anapata haki yake kwa mujibu wa sheria za ardhi zinavyosema .

 

Juliasi Mgeni ni mmoja ya wananchi wa Kijiji cha Isupilo alisema kuwa mwenyekiti wa Kijiji hicho Joakimu kisinini ndio chanzo cha migogoro ya ardhi.

 

Mgeni alisema kuwa mwenyekiti huyo amejimilikisha ardhi ya wananchi kwa kutumia madaraka aliyokuwa nayo.

 

Alisema kuwa watu wa ardhi wanachochea mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na mwekezaji kwa kutoa taarifa tofauti tofauti kila mara.

  

Mgeni alisema kuwa hawaridhishwi na maamuzi ya ofisi ya ardhi ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa hivyo mkuu wa wilaya anaombwa kutatua mgogoro huo.

 

alimalizia kwa kusema shamba la muwekezaji kampuni ya Overland linahekari 1262 huku hekari 953 hazina mgogoro wowote na hekari 296 ndio zinamgogoro ambao kwa kiasi kikubwa ndio chanzo cha tuhuma hizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.