Habari za Punde

DC Moyo Amedhamiria Kutokomeza Ujangiri katika Hifadhi ya Ruaha

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kijiji cha Kitisi kata ya Idodi juu ya umuhimu wa kutunza na kuwalinda wanyama pori wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha 
Mradi wa Lion landscapes Wiston Mtandamo akiongea na wananchi wa kijiji cha Kitisi kata ya Idodi juu ya umuhimu wa kutunza na kuwalinda wanyama pori wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kitisi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa kupewa elimu ya kuwatunza na kuwalinda wanyama pori wa Hifahdi ya Taifa ya Ruaha

Na Fredy Mgunda, Iringa.

MKUU wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ametangaza vita na mwananchi yeyeto anajihusisha na ujangiri wa wanyama pori katika hifadhi ya Taifa Ruaha hiyo imetokana na kuongezeka kwa vitendo vya ujangiri katika Vijiji ambavyo vinaizunguka hifadhi hiyo.


Akizungumza wakati wa utiaji wa saini Mkataba wa makubaliano ya katika uhifadhi na usimamizi, maendeleo ya jamii na kukutunza mali hai zote baina ya wananchi wa Kijiji cha Kitisi na Lion landscapes katika kata ya Idodi wilaya ya Iringa, Moyo alisema kuwa ujangiri umekuwa unaongezeka kila siku.


Moyo alisema kuwa serikali itawafungulia mashitaka viongozi wa Serikali za vijiji wakiwemo wenyeviti watakaozembea katika vita ya kutokomeza ujangili katika maeneo yao huku akiwataka kuunda vikundi maalum vya ulinzi shirikishi. 


Alisema kuwa umeanza kuongezeka kwenye Vijiji ambavyo vinapakana na hifadhi ya Taifa Ruaha kiasi kwamba kunahatarisha uhai wa wanyama pori ambao wamehifadhiwa katika hifadhi hiyo. 


Moyo alisema kuwa serikali ya wilaya ya Iringa haitamfumbia macho mtu yeyeto yule ambaye atakutwa na kesi ya ujangili basi ajue maisha yake yataishia Gerezani. 

Aidha mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliwapongeza Lion landscapes kuendelea kuwalinda wanyama pori na kuviwezesha kiuchumi Vijiji ambavyo vipo kwenye mradi huo.

 

Awali meneja wa Mradi wa Lion landscapes Wiston Mtandamo alisema kuwa bado wananchi wa Kijiji cha Kitisi wanaendelea na ujangili kwa kuuwa wanyama mbalimbali kwa ajili ya kupata kitoeo,kutumisha Milla na wengi kwa ajili ya biashara haramu ya kuuza nyama pori mtaani kinyume na sheria za nchi.


Mtandamo alisema kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu wamekamata mitego tisa ambayo ilikuwa imetegwa porini kwa ajili ya kuwanasa wanyama pori Jambo ambalo linasababisha kutoweka kwa baadhi ya wanyama pori.


Kwa upande wake diwani wa kata ya mapogolo Julias Mbuta amewahimiza wananchi wa kijiji hicho na vijiji vyote vinavyounda kata ya Idodi kuhakikisha wanashirikiana Mradi wa Lion landscapes na serikali katika kuendeleza uhifadhi kwa manufaa ya Vijiji vyote vilivyo jirani na vilivyo nje ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.