Habari za Punde

Ziara ya Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma

MWENYEKITI wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mst. Hamisa Kalombola, akizungumza na menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) wakati wa ziara ya Makamishna wa Tume Utumishi wa Umma katika Mamlaka hiyo jijini Dodoma jana. 
MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph, akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mst. Hamisa Kalombola pamoja na Makamishna katika vituo vya kusukumia maji (booster station) Mzakwe wakati wa ziara ya Makamishna wa tume katika Mamlaka hiyo jijini Dodoma jana. 

MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph, akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mst. Hamisa Kalombola (katikati) pamoja na Makamishna kuhusu ukubwa wa visima na aina ya pampu zinazotumika wakati wa ziara ya Makamishna wa tume katika Mamlaka hiyo jijini Dodoma jana.
MWENYEKITI wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mst. Hamisa Kalombola (wa tatu kulia) pamoja na Makamishna wakimsikiliza Mwandisi wa Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Peter Shemwelekwa, akielezea mfumo wa kieletroniki wa uzalishaji maji wakati wa ziara ya Makamishna wa tume katika Mamlaka hiyo jijini Dodoma jana. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph.
MWENYEKITI wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mst. Hamisa Kalombola, akizungumza na menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) wakati wa ziara ya Makamishna wa Tume Utumishi wa Umma katika Mamlaka hiyo jijini Dodoma jana. (Picha na Mpigapicha Wetu)

MWENYEKITI wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji mstaafu Hamisa Kalombola ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuendelea kuwa wabunifu ili kuhakikisha majisafi na salama yanapatikana wakati wote.

Ameyasema hayo jana wakati wa ziara ya kikazi ya makamishna wa tume hiyo katika ofisi za DUWASA ambapo alizungumza na menejimenti ya Mamlaka hiyo.

“Mamlaka yenu iendelee kufanya tathmini ya mipango yake ili uwekezaji unaofanyika uwe na matokeo chanya na lengo la Serikali la kuwaletea watanzania ustawi wa maendeleo liweze kufikiwa,” alisema Jaji Mstaafu Hamisa

Pia, aliwataka watumishi kujiepusha na vitendo vya utovu wa nidhamu, uzembe, wizi, ubadhilifu, uombaji wa rushwa ili wananchi wapate huduma bora.

“Mtaweza kujiepusha kutenda makosa kwa kuhakikisha wakati wote mnatekeleza majukumu yenu kwa kuzingatia sheria, kanuni na utaratibu,” alisema Jaji mstaafu Hamisa

Naye Kamishina wa Tume hiyo, Susan Mlawi alisema wao kama tume wana jukumu la kuweza kufahamu mazingira ambayo watumishi wanafanya kazi ikiwa sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma zinazingatiwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph alisema kwa sasa miradi ambayo inahitajika kutekelezwa kwa uharaka ni kupeleka maji mjini Dodoma kwa kutumia bwawa la Mtera wakati ikisubiriwa maji ya Bwawa la Farkwa au ziwa Victoria ambayo yanaweza kuchukua muda mrefu.

Alisema mahitaji ya maji kwa Jiji la Dodoma ni lita milioni 133 kwa siku lakini yanayozalishwa kwa sasa ni lita milioni 67 hivyo kuna upungufu wa lita milioni 66  lakini mradi wa maji kutoka Bwawa la Mtera unatarajia kuingia lita 68 na kufanya jiji liwe na lita 201 milioni ambayo yatatosha kwa matumizi walau kwa miaka 13 ijayo.
--
Halima Kambi
Ass. Communication Officer
Dodoma Urban Water Supply and Sanitation Authority (DUWASA)
P.O. BOX 431 Dodoma
Dar es Salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.