Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Aondoka Nchini Akielekea Nchini Omani kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Nne Nchini Humo leo 11-10-2022

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akielekea Nchini Oman kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Nne Nchini humo leo 11-10-2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakisalimiana na kuagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea Nchini Oman kwa ziara ya siku nne ya Kikazi Nchini humo leo 11-10-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimia na kuagana na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea Nchi Oman kwa ziara ya Kikazi ya Siku nne Nchini humo leo.11-10-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwapungia mkono na kuwaaga Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Siasa, wakati akiondoa Nchini akielekea Nchini Oman kwa ziara ya Kikazi ya Siku Nne Nchini humo leo 11-10-2022

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Ali Mwinyi, asubuhi ya  leo Jumanne tarehe 11 Oktoba ameondoka Zanzibar kuelekea Oman kwa ziara ya kikazi ya siku nne kufuatia mwaliko wa Mfalme wa nchi hiyo. 

Rais Dk Hussein Ali Mwinyi,  katika ziara hiyo ameambatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi, baadhi ya Mawaziri na Wakuu wa Idara na Mashirika mbalimbali ya Serikali na wafanyabiashara.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar , Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi aliagwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman,  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman  Abdullah na Viongozi mbalimbali wa Serikali na vya Siasa, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wa SMZ na SMT.

Akiwa nchini Oman Dk. Mwinyi atakutana na Mfalme wa Oman, Sultan Haitham bin Tariq, Wafanyabiashara, Wana-Diaspora na atatembelea miradi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.