Mamlaka ya kuzuia Rushwa na
Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kwa kushirikiana na Afisi ya Mkurugenzi wa
Mashtaka (DPP), Tarehe 29/12/2022 imewafikisha Mahakama Kuu Tunguu-Zanzibar
Watuhumiwa Kumi na Nne (14) kwa makosa mbali mbali ya Rushwa na Uhujumu Uchumi
kinyume na Sheria ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, nambari 1 ya
mwaka 2012.
Watuhumiwa hao pamoja na Kesi
zao ni:-
1. KESI
NAMBARI 126/2022
WATUHUMIWA
1. KASSIM
JUMA KHAMIS (52) mkaazi wa TOMONDO-Zanzibar aliyekuwa Mshika Fedha Mkuu wa
Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU)
2. MACHANO
KOMBO KHAMIS (42) mkaazi wa KIJICHI -Zanzibar aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa
Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU)
3. ALI OTHMAN YUSSUF (43) mkaazi wa
Mjini-Zanzibar aliyekuwa mwingiza taarifa kwenye mfumo wa malipo Jeshi la
Kujenga Uchumi (JKU)
4. KHAMIS
ALI KHAMIS (37) Mkaazi wa CHUKWANI -Zanzibar aliyekuwa Msimamizi wa Mfumo
wa Malipo (System Administrator) wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar
Watuhumiwa
hao wanashtakiwa kwa kosa la:- Ubadhirifu wa Mali na Mapato Tsh. 314,307,950/-
kinyume na Kifungu cha 42(2) (b) cha Sheria ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi
Zanzibar, nambari 1 ya mwaka 2012.
Kesi
imesomwa mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Mh. Rabia Hussein Mohamed ambapo
Watuhumiwa hao wamekana makosa yao na wamepewa dhamana ya Bondi ya Tsh.
20,000,000/= kila mmoja pamoja na wadhamini wao. Isipokuwa Mtuhumiwa KASSIM
JUMA KHAMIS ambae amenyimwa dhamana yake.
Kesi
hii itatajwa tena 10/01/2023 kwa ajili ya uamuzi mdogo.
2. KESI NAMBARI 129/2022 WATUHUMIWA
1. ALI KHAMIS ALI (43) mkaazi wa
MAMBOSASA-Zanzibar aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango
Zanzibar.
2. KHAIRAT
G. SANGA (38) mkaazi wa FUONI-Zanzibar aliyekuwa Msaidizi Mhasibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar.
3. FATMA ABDALLA HASSAN (42) mkaazi wa
MWERA-Zanzibar aliyekuwa Msaidizi Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar.
4. TALIB
ABDULMANAN AMEIR (50) mkaazi wa KAMA-Zanzibar aliyekuwa Mshika Fedha Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar.
5. KHAMIS ALI KHAMIS (37) Mkaazi wa
CHUKWANI -Zanzibar aliyekuwa Msimamizi wa Mfumo wa Malipo (System
Administrator) wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar
Watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa makosa ya :-
1. Ubadhirifu wa Mali na Mapato kinyume na
Kifungu cha 42(2) (b) cha Sheria ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar,
nambari 1 ya mwaka 2012.
2.
Kutumia vibaya Mali kinyume na Kifungu cha 43 cha Sheria ya Kuzuia Rushwa na
Uhujumu Uchumi Zanzibar, nambari 1 ya mwaka 2012.
3.
Matumizi Mabaya ya Ofisi kinyume na Kifungu cha 53 cha Sheria ya Kuzuia Rushwa
na Uhujumu Uchumi Zanzibar, nambari 1 ya mwaka 2012.
Watuhumiwa
hao kati ya mwaka 2014 na 2015 kwa makusudi waliuchezea Mfumo wa Malipo wa
Serikali “EPICO 7” na kujipatia bila ya halali jumla ya Tsh. 81,940,228/- na
kusababisha hasara kwa Serikali.
Kesi
hii imesomwa mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Mh. Rabia Hussein Muhamed ambapo
Watuhumiwa wamekana makosa yao na wamenyimwa dhamana hadi terehe 10/01/2023 kwa
ajili ya uamuzi mdogo.
3.
KESI NAMBARI 127/2022 WATUHUMIWA
1. KHATIB
ALI HAMDU (48) mkaazi wa CHUKWANI-Zanzibar aliyekuwa Mhasibu Mkuu Kikosi
Maalumu cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM).
2. MUHAMMED MAKAME ALI (40) mkaazi wa
SHARIFUMSA Zanzibar aliyekuwa Muingizaji taarifa kwenye Mfumo wa Malipo Kikosi
Maalumu cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM).
3. KHERI
ALI ABDALLA (41) mkaazi wa FUONI -Zanzibar aliyekuwa Mtunza Ghala Kikosi
Maalumu cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) Watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa
makosa:-
1. Matumizi Mabaya ya Ofisi kinyume na Kifungu
cha 53 cha Sheria ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, nambari 1 ya
mwaka 2012.
2.
Ubadhirifu wa Mali na Mapato Tsh. 20,000,000/- kinyume na Kifungu cha 42(2) (b)
cha Sheria ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, nambari 1 ya mwaka
2012.
Kesi
hii imesomwa mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Mh. Rabia Hussein Mohamed ambapo
Watuhumiwa hao wamekana makosa yao na wamepewa dhamana ya Bondi ya TSh.
20,000,000/- kila mmoja na wadhamini wao wawili TSh. 10,000,000/- kila mmoja.
Kesi hii itatajwa tena 10/01/2023 kwa ajili ya
uamuzi mdogo.
4. KESI NAMBARI 128/2023 WATUHUMIWA
1. MSANIFU SHAKA JUMA (39) mkaazi wa
Mjini -Zanzibar
2. MOHAMMED MWALIMU PONGWA (28) mkaazi
wa SHAKANI-Zanzibar wote ni Watumishi wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kwa
nafasi ya Wauzaji umeme katika Kituo cha kuuzia umeme Makunduchi. Watuhumiwa
hao wanashtakiwa kwa makosa ya:-
1. Matumizi Mabaya ya Ofisi kinyume na Kifungu
cha 53 na 61 cha Sheria ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, nambari 1
ya mwaka 2012.
2.
Ubadhirifu wa Mali na Mapato kinyume na kifungu cha 42(1)(a) cha Sheria ya
Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, nambari 1 ya mwaka 2012.
Watuhumiwa
hao bila ya halali walijipatia Tsh. 142,992,909/- kwa kutowasilisha fedha hizo
Benki baada ya mauzo ya umeme katika kituo cha Makunduchi. Kesi hii imesomwa
mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Mh. Mohamed Ali Mohamed ambapo Watuhumiwa hao
wamekana makosa yao na wamepewa dhamana kila mmoja na wadhamini wao wawili
bondi ya TSh. 50,000,000/- Kesi hii itatajwa tena 06/01/2023 kwa ajili ya
kuwasilisha maelezo ya mashahidi.
5. KESI NAMBARI 125/2022 MTUHUMIWA
1. SHEHE
ALI SHEHE (41) mkaazi wa TOMONDO -Zanzibar Mfanyakazi wa Wizara ya
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Zanzibar.
Mtuhumiwa
anashtakiwa kwa kosa la :- Kuomba na kupokea Rushwa ya Tsh. 650,000/= pamoja na
Matumizi Mabaya ya Ofisi kinyume na Kifungu cha 53, 36(3)(a) na 61 cha Sheria
ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, nambari 1 ya mwaka 2012. Kesi hii
imesomwa mbele ya Jaji wa Mahkama Kuu Mh. Mohamed Ali Mohamed ambapo Mtuhumiwa
amekana kosa lake na amepewa dhamana ya bondi ya Tsh. 500,000/= na wadhamini
wawili.
Kesi
hii itatajwa tena 06/01/2023 kwa ajili ya kuwasilisha maelezo ya mashahidi.
IMETOLEWA
NA: Kitengo cha Uhusiano, Mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar
(ZAECA
No comments:
Post a Comment