Habari za Punde

Tanzania na Cuba Kuazisha Maeneo Mapya ya Ushirikiano

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb). akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt.Stergomena Tax akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Mhe. Yordenis Despaigne Vera yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Mhe. Yordenis Despaigne Vera wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara na Ubalozi mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Tanzania na Cuba zimeaahidi kuaanzisha maeneo mapya ya ushirikiano katika nyanja za afya (chanjo), biashara na uwekezaji, uzalishaji wa mbolea na kilimo.

Ahadi hiyo imetolewa katika kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Tax amesema kuwa kuanzishwa kwa maeneo mapya ya ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba kutasaidia kuimarisha ushirikiano uliodumu kwa takribani miaka 60 pamoja na kunufaisha wananchi wa mataifa yote mawili kiuchumi.

“Tunaamini kuwa kuanzishwa kwa maeneo mapya ya ushirikiano kutawanufaisha wananchi wa mataifa yote mawili kiuchumi, Tanzania inaahidi kuendelea kushirikiana na Cuba kidiplomasi kwa maslahi mapana ya pande zote mbili,” Alisema Dkt. Tax

Mbali na maeneo mapya ya ushirikiano, Tanzania imekuwa ikishirikiana na Cuba katika sekta za afya, elimu, utalii, ulinzi na viwanda.

Kwa upande wake Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendeleza ushirikiano mzuri na imara baina yake na Serikali ya Cuba.

“Tanzania imekuwa ikishirikiana na Cuba kwa muda mrefu na uhusiano huo umekuwa imara tangu ulipooasisiwa na viongozi wakuu wa Mataifa hayo Hayati Fidel Castor na Hayati Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,” Alisema Balozi Vera.

Cuba inaahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kuimarisha misingi ya kidiplomasia kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili. “Ni wakati muafaka sasa Cuba na Tanzania kuimarisha ushirikiano na kuhakikisha unakuwa na mafanikio ya kiuchumi kwa manufaa ya mataifa yote mawili,” aliongeza Balozi Vera.  
 
Tanzania ilianzisha uhusiano wake wa kidiplomasia na Cuba mwaka 1963 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.