Habari za Punde

Protokoli ni Sehemu ya Uhusiano: Balozi Kalaghe

Balozi (Mstaafu), Mhe. Peter Kallaghe, akizungumza na washiriki.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID                                                      

PROTOKALI ni sehemu ya Uhusiano, Balozi (Mstaafu), Mhe. Peter Kallaghe amewaambia Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali (TAGCO) wanaohudhuria Kikao Kazi cha 18 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam Machi 28, 2028.

Balozi Kalaghe ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada ya Protokali (Protocol) kwa wajumbe wanaoshiriki kikao hicho cha siku tano kilichoanza Machi 27, 2023.

Kazi ya tasnia yenu ni kufungua milango ambayo imefungwa, tabia ni moja ya njia bora ya kufungua milango iliyofungwa, alisema.

Aliwaeleza misingi mbalimbali ya kuzingatia katika Protokali ili kuonyesha ustaarabu katika ofisi wanazozitumikia.

Baadhi ya misingi ya Protokali aliyowaeleza Maafisa hao wapatao 600 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, ni dhima ya kuwashauri viongozi wao katika ushiriki wa matukio mbalimbali ndani ya ofisi na j nje ya ofisi.

Alisema pamoja na wajibu mwingine Maafisa hao wanawajibu wa kuwashauri viongozi wao kuhusu  kuheshimu mialiko, pia muda, kwani hiyo ni ishara ya kuonyesha heshima ya shughuli husika .

“ Lazima uonyeshe ustaarabu (etiquette), kwa kujua mambo ambayo kwa utamaduni wa sehemu fulani linakubalika au halikubaliki.” Alibainisha na kuongeza..

Aliwaeleza umuhimu wa uchaguzi wa mavazi wanayovaa wanapotekeleza majukumu yao ya kikazi na kuwaeleza kuepuka mavazi yanayopiga kelele (shouting collors).

“Unavyovaa ni sehemu ya weledi wako, kuelewa nguo gani unavaa na kwa wakati gani.” Alifafanua.

Akieleza zaidi Balozi Kallaghe ambaye ni mbobezi katika fani ya Mawasiliano alisema wanapaswa kujua utaratibu wa ukaaji (Setting arrangement) kwa viongozi wao, namna ya kuzungumza, kutamka majina kwa usahihi.



Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mindi Kasiga akizunguzma kwenye Kikao hicho.

Balozi Kallaghe akiteta jambo na Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sara Kibonde
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele ambaye ni Mwenyekiti wa Kikao, akiongoza majadiliano.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa akijibu baadhi ya hoja za washiriki.
Bw. Kakele na Bw. Msigwa wakiteta jambo
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Misiime akifuatilia kwa makini mafunzo.









No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.