Sehemu
ya wajumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na wale kutoka Ubalozi wa Norway
wakifuatilia kikao cha majadiliano ya ushirikiano baina ya Serikali za Tanzania
na Norway kilichofanyika katika za Ofisi ya Makamu wa Rais, Mji wa Serikali
Mtumba Jijini Dodoma leo Jumanne Machi 21, 2023.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Bi. Mary Maganga
akibadilishana mawazo na ujumbe wa maofisa waandamizi kutoka kutoka Ubalozi wa
Norway mara baada ya kumalizika kwa kikao cha majadiliano ya ushirikiano baina
ya Serikali za Tanzania na Norway kilichofanyika katika za Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Bi. Mary Maganga (mwenye
suti mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa maofisa
waandamizi kutoka kutoka Ubalozi wa Norway mara baada ya kumalizika kwa kikao
cha majadiliano ya ushirikiano baina ya Serikali za Tanzania na Norway
kilichofanyika katika za Ofisi ya Makamu wa Rais, Mji wa Serikali Mtumba Jijini
Dodoma leo Jumanne Machi 21, 2023.
Hayo
yamesemwa leo Jumanne (Machi 21, 2023) Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Mazingira
Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Andrew Komba wakati wa kikao cha majadiliano ya
ushirikiano baina Serikali hizo mbili kilicholenga mikakati ya Utekelezaji wa Miradi ya uhifadhi wa mazingira na
kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Akiwasilisha
salamu za Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Bi.
Mary Maganga, Dkt. Komba amesema Serikali ya Norway imekuwa na ushirikiano wa
muda mrefu na Tanzania katika sekta mbalimbali na kuongeza kuwa kwa sasa
masuala ya mazingira yanazidi kupewa kipaumbele katika ushirikiano baina ya
nchi hizo mbili.
Dkt.
Komba ameelezaa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana Norway katika
masuala ya usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali zinazopatikana baharini
bila kuathiri hifadhi ya mazingira na kuanisha hatua mbalimbali zilizofikiwa
katika juhudi za uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.
Akifafanua
zaidi Dkt. Komba ameitaja moja ya miradi inayotekelezwa na Serikali ya Norway kupitia
Shirika la Maendeleo la Norway NORAD ni pamoja na Mradi wa kujengea uwezo
Taasisi zinazojishughulisha na masuala ya mazingira ili kupunguza hewa ukaa
inayosababishwa na ukataji miti na uhalibifu wa Misitu (REDD+ READY)
unaotekelezwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Aidha
Dkt. Komba amebainisha moja ya manufaa ya utekelezaji wa Mradi wa (REDD+ READY)
ni pamoja uimarishwaji wa mifumo ya usimamizi endelevu ya matumizi ya ardhi kwa
ajili ya shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo ambapo kumewezesha kupungua kwa uhalibifu
wa mazingira ikiwemo ukataji miti na uchomaji wa misitu.
“Mabadiliko
ya tabianchi yapo na upo uwezekano wa kukabiliana nayo, kwa kuwa ardhi bado ipo
tunaweza kurejesha uoto wa asili ili vizazi vijavyo kunufaika. Serikali
imeendelea kuchukua hatua muhimu za
uhifadhi wa mazingira kwa kuendelea kushirikiana na wadau na wafadhili
mbalimbali ikiwemo NORAD” amesema Dkt. Komba.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa masuala ya mabadiliko ya Tabianchi kutoka Ubalozi wa
Norway, Bw. Odd Arnesen ameipongeza Tanzania kwa kuchukua hatua na jitihada mbalimbali
za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambazo zimekuwa zikihatarisha
usalama wa chakula.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na viongozi, maofisa waandamizi na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment