Habari za Punde

Uzinduzi wa Bohari ya Mafuta Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud, akizungumza katika eneo la kushushia mafuta katika Bandari Jumuishi Mangapwani wakati wa hafla ya ufunguzi wa Bohari ya Mafuta ya Kampini ya United Petrolium (UP) Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 4-3-2023. na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Waziri wa Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Shaibu Hassan Kaduara na (kushoto kwa Rais) Bw Abubakar Bakressa na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe. Dkt.Khalid Salum Mohammed.
 
Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw.Nahaat Mohammed Mahfoudh akitowa maelezo ya kitaalum kuhusina na eneo la Bandari Jumuishi Mangapwani Zanzibar wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Bohari ya Mafuta ya Kampuni ya United Pertrolium (UP) katika eneo la Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni ya Mafuta ya United Petroleum (UP) Bw.Collins Chemngorem akizungumza na kutowa maelezo ya Kitaalum, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Bohari ya Mafuta Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 4-3-2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud wakati katika eneo la Bandari Jumuishi Mangapwani wakati wa hafla ya ufunguzi wa Bohari ya Mafuta ya Kampuni ya United Petroleum (UP).


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.