Habari za Punde

ELIMU YA MARADHI YASIAMBUKIZWA YATOLEWA MAJUMBANI

Maafisa wa Afya walipokuwa wakitoa huduma za Afya katika ngazi ya Jamii kwa Wagonjwa wa Maradhi yasioambukiza huko Koani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kaskazini Unguja
Afisa kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Hafidh Abdurahman Seif akizungumza na kikundi cha Wagonjwa wa Maradhi yasioambukiza  wakati alipokua akitoa elimu juu ya maradhi hayo kabla ya kuanza kwa zoezi la utoaji wa  huduma za Afya  ngazi ya jamii lililoandaliwa na  Wizara ya Afya wakishirikiana na PharmAccess international  huko  Koani Wilaya ya Kat
Mwana kikundi cha Wagonjwa wa Maradhi yasioamhmbukiza Bimkasi akizungumza wakati alipokua Akitoa ushuhuda wa mabadiliko ya Afya yake mara baada ya  kufanya mabadiliko ya  mlo, wakati wa zoezi la utoaji wa huduma za Afya ngazi ya jamii lililofanyika Koani Wilaya ya kati.PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR

Na Fauzia Mussa -Maelezo Zanzibar

Jamii imeshauriwa kutumia mlo uliokamiki ili kuepuka maradhi yasioambukiza ambayo yameshika kasi katika jamii.

Ameyasema hayo Afisa kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Hafidh Abdurahman Seif wakati alipokua akitoa elimu  kwa wagonjwa wa maradhi yasioambukiza katika hafla ya wa utoaji wa huduma za Afya kwa ngazi ya jamii  huko Koani Wilaya ya Kati Unguja

Ameeleza kuwa maradhi  ya kuambikiza yamekua yakiongezeka  kwa kasi zaidi  kutokana na jamii  kutokuwa tayari kufanya mabadiliko  ya mfumo wa chakula

Alisema ulaji usiozingatia makundi ya mlo ni sababu inayopelekea maradhi hayo kuongezeka hivyo ameishauri jamii kupunguza matumizi ya vyakula vya uwanga na kutumia matunda kwa wingi.

"Nibora Kula chakula Bora nasio Bora chakula, tuachane na vyakula vya kusindikwa vimekosa virutubisho ,sasa tutumie vyakula vyetu vyaasili ambayo hata gharama yake nindogo"alishauri

Alifahamisha kuwa kiafya kwa siku inatakiwa kutumia uwanga ujazo wa mkono , mboga mboga kwa wingi na mafuta yasiozidi vijiko viwili vya chakula hivyo ameiasa jamii kuwa na   Utamaduni  huo ili kupunguza ongezeko la maradhi hayo.

"Kitu chochote kinapoongezeka katika mwili ni sumu, si uwanga,mafuta ,sukari wala chumvi ivyo tujitahii kupunguza matumizi ya vitu hivi kwani ni miongoni mwa sababu za maradhi haya"alifahamisha

Aliongeza kuwa maradhi yasioambukiza yamekua yakiendelea kuongezeka siku Hadi siku kutokana na jamii kutokua tayari kuachana na  matumizi ya  vichocheo vya maradhi hayo sambamba na urithi kutoka kwa familia.

Aidha amefahamisha kuwa  uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupitiliza umetajwa  kusababisha maradhi yasioambukiza ikiwemo pumu na  saratani ya mapafu .

Afisa huyo ameeleza kuwa jamii haina mazowea ya kufanya mazoezi ya viungo jambo ambalo linasababisha ongezeko la wagonjwa wa maradhi hayo siku hadi siku.

Amesema mazoezi ni njia moja wapo ya kutoa takataka mwilini hivyo ni vyema kufanya mazoezi ya viungo angalau nusu saa kwa siku kwani kutasaidia kupunguza ongezeko la maradhi hayo

Hata hivyo Afisa huyo aliishauri jamii kujitokeza katika  vituo vya Afya  kufanyiwa vipimo  mara kwa mara ili kuangalia Afya zao dhidi ya maradhi yasioambukiza  .

Nao waathirika wa maradhi yasioambukiza wameishukuru Wizara ya Afya  na Pharm Access kwa kuwafikia na  kuwapatia  elimu juu ya maradhi hayo sambamba na kuwasogezea huduma za Afya katika ngazi ya jamii.

"Tangu nipate muamko na elimu nimebadilika nakunywa uji wa mtama saa Saba nakula dona ,mboga na supu ya dagaa,usiku nakula mkate wa atta nikikosa narudia uji basi alhamdulillah kwa sasa naendelea vizuri nafika shamba kulima"alielezea Bimkasi miongoni mwa wagonjwa wa sukari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.