Habari za Punde

WAZIRI BALOZI DKT. PINDI CHANA ACHANGIA MABATI 144 KWA SHULE YA SEKONDARI YAKOBI.

 

Na Mwandishi wetu

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe kupitia Chama Cha Mapinduzi, (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amechangia vifaa mbalimbali vya ujenzi yakiwemo mabati  144 kwa shule ya Sekondari Yakobi iliyopo Mkoani Njombe.

Akikabidhi mabati hayo Aprili 25, 2023 mkoani hapo Mhe.Balozi Dkt. Pindi chana amesema anaunga mkono jitihada za Serikali katika kuweka mazingira bora kwa Wanafunzi kupata elimu ambayo ndiyo nguzo katika maisha yao.

"Mnapokua darasani hakikisheni mnawasikiliza walimu, mnauliza maswali I'll katika maeneo ambayo hamjaelewa, lakini zingatieni nidhamu, tabia na siha njema" Amesisitiza Mhe. Chana.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekabidhi pia mipira pamoja na Jezi kwa Wanafunzi wa shule hiyo akitoa wito kwa Shule  hizo zisibadilishe Matumizi ya viwanja vya michezo pamoja na maeneo ya shughuli za Utamaduni na Sanaa.

Amewaasa walimu wa Shule hiyo waheshimu ratiba za vipindi vya michezo na kuwapa nafasi Wanafunzi kucheza huku akiwataka Wanafunzi hao waheshimu Mila na Desturi za Kitanzania na kuacha tabia za kigeni ambazo  zinazokiuka maadili ya Mtanzania ikiwemo mapenzi ya jinsia moja.

Mmoja wa Wanafunzi wa Shule hiyo, amenshukuru Waziri Balozi Dkt.Pindi Chana  kwa vifaa hivyo ambavyo watavitumia kuongeza maarifa, kukuza na kuendeleza vipaji vyao.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.