Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Ahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Jukwaa la Uchumi Doha Qatar

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi leo tarehe: 23 Mei 2023 amehudhuria ufunguzi wa Jukwaa la Uchumi 

ambapo viongozi mbalimbali duniani wamehudhuria ufunguzi huo akiwemo Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Kabla ya ufunguzi wa Jukwaa hilo Dk. Mwinyi alizungumza na Mhe. Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Amir wa Taifa la Qatar.

Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Qatar hutumia Jukwaa hilo la biashara kila mwaka kujitangaza kiuchumi na kukaribisha wawekezaji mbalimbali.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.