Habari za Punde

MYSOL Yawafikia Wazanzibar

Waziri wa Maji,Nishati na Madini Shaibu  Hassan Kadura akisalimiana na watendaji wa kampuni ya MY SOL wakati alipofika kuzindua duka la vifaa vya sola vinavyosambazwa na Kampuni hiyo huko Gulioni Makadara Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Waendesha Pikipiki Bodaboa wakisherehesha hafla za Uzinduzi wa Duka la My Sol Golinoni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar. 
Waendesha Pikipiki Bodaboa wakisherehesha hafla za Uzinduzi wa Duka la My Sol Golinoni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar. 
Kikundi cha ngoma kutoka magereza wakitoa Burudani katika hafla ya uzinduzi wa duka la kuuzia vifaa vya sola vya  kampuni ya (MY SOL) huko Gulioni Makadara Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi
Waziri wa Maji,Nishati na Madini  Shaibu Hassan Kadura  akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la vifaa vya sola kutoka kampuni ya MY SOL huko Gulioni Makadara Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya MY SOL Godfrey Mugambi akitoa maelezo mafupi kuhisana na bidhaa za sola ambazo zitauzwa katika duka lao lililozinduliwa rasmi na Waziri wa Maji,Nishati na Madini Shaibu Hassan Kadura huko Gulioni Makadara Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana  Mustafa akizungumza machache na kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Maji,Nishati na Madini  Shaibu Hassan Kadura kuzindua duka la vifaa vya sola la Kampuni ya MY SOL huko Gulioni Makadara Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi
Waziri wa Maji,Nishati na Madini Hassan Kadura  akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa duka la kuuzia vifaa vya sola vya  kampuni ya (MY SOL) huko Gulioni Makadara Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Na Rahma Khamis Maelezo  Zanzibar.   

Mkurugenzi Mkuu  wa Kampuni ya My Sol  Godfrey Mugambi amesema wapo tayari kushirikiana na Serikali  kuchangia upanuzi wa ufikishaji umeme maeneo ambayo hayajafikiwa  ili wananchi wapate huduma hiyo.

Ameyasema hayo huko Gulioni wakati wa uzinduzi wa Tawi la Kampuni hiyo na kusema kuwa uzinduzi wa tawi hilo ni mikakati ya  kuwawezesha watu milioni 20 kupata  huduma za nishati safi na salama Barani Afrika.

Amesema nishati ya umeme ni muhimu kwa kila Taifa kwani ni njia moja wapo ya kuleta maedeleo katika  nchi hivyo wameamua kuja na  kuuunga mkono Serikali ya Zanzibar ili  kufaninisha azma ya kuwafikishia huduma wananchi wake.

Amefahamisha kuwa ni heshima kubwa kuona  Viongozi wa Serikali  wanapambana katika kuhakikisha wanawahudumia  na kuwafikishia huduma  za nishati ya umeme sehemu ambazo hazijafikiwa na hudma hiyo .

Pia amesema kampuni itatoa mafunzo kwa zaidi a watu 150 na kunufaisha zaidi a wananchi laki saba ili kuhakikisha wananchi wa uwelewa na ufaahamu wa kutumia mhuduma hiyo .

Hata hivyo Mkurugenzi ameeleza kwamba  wamedhamiria kuchukua jitihada za makusudi kuinua  juhudi za Serikali katika kupambana na harakati za kuleta maendeleo Mjini na Vijijini kwa  kupata huduma za nishati mbadala.

Mapema Waziri wa Maji,Nishati na Madini Mhe, Shaibu Hassan Kaduara wakati akizindua duka hilo amesema umeme wa sola ni rahisi zaidi Ulimwenguni kwani una unafuu katika maisha.

Amesema umeme wa sola ni umeme kama umeme unaotumiwa majumbani  kwani inapendeza zaidi kuutumia  na kurithisha vizazi vijavyo  ili kuhifadhi mazingira.

Aidha Waziri ameitaka kampuni hiyo kufanya kazi zao kwa uhuru bila ya wasiwasi kwani wananchi wa Zanzibar wanahitaji maendeleo na kusonga mbele zaidi  kupitia miradi mbalimbali.

Waziri Kaduara  ameeleza kuwa kazi ya kuleta maendeleo si ndogo kwani Rais Mwinyi anakesha usiku na mchana kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ikiwemo umeme hivyo amewashauri wananchi kutumia fursa hiyo ili kupunguza gharama za matumiz ya nishati ya umeme.

"Ikiwa kuna tatizo kwa mtu yeyote katika matumizi ya umeme asione shida kutumia umeme wa sola kwani unapatikana kwa urahisi na wala hauna gharama kubwa isipokuwa inategemea na matumizi ya mtu mwenyewe", alisema Waziri.

Aidha amefahamisha kuwa kuna taa za sola ambazo zinaweza kutumwia bila ya matatizo kwani kuna faida nyingi zinazopatika katika umeme huo ikiwemo kupunguza gharama ukilinganisha na umeme wa kawaida.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Idrisa Kitwana Mustafa amemtka Mkurugenzi wa Kampuni hio kuzingatia vijana wazawa wakati wanapotaka kutoa ajira katika duka hilo.

Kwa upande wao wananchi wameishukuru Kampuni hiyo kwa kuwasogezea huduma karibu kwani itawasaidia kuwapunguzia gharama kwani baadhi ya matumizi ya vifaa vya umeme hawamudu kutokana na hali zao za maisha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.