Habari za Punde

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Balozi. Dkt. Pindi Chana Ashuhudia Tanzania Ikipata Udshindi Dhidi ya Timu ya Italia Mpira wa Wavu Mchezo wa Olimpiki Maalum Berlin

 

Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Tanzania Balozi Dkt.Pindi Chana akiwa na baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Tanzania wanaoshiriki Michezo ya Olimpiti Maalumu Berlin Nchini Ujerumani. 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana mapema leo Juni 19, 2023 ameshuhudia Timu ya Tanzania ya Olimpiki Maalum ya Mpira wa Wavu ikiitandika bila huruma timu ya Italia kwa pointi 25 - 10 katika mchezo wa awali wa mchujo ( Preliminary Stage) na kufuzu hatua ya pili ya mchujo.

Michezo ya Olimpiki Maalum imeanza leo ambapo pia Mwanariadha Mtanzania Mathias Makanyaga amefanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye mbio za Mita 800  na hivyo kufuzu hatua ya fainali.

Katika mchezo mwingine Timu ya wanaume ya Mpira wa Wavu imepoteza kwa point 17- 16 dhidi ya timu ya Botswana ambapo pia imefanikiwa kufuzu hatua inayofuata ya mchujo.

Michezo hiyo inayofanyika katika uwanja wa Messe Berlin ma  inatarajiwa kuendelea kesho kwa hatua mbalimbali ambapo mchezaji wa riadha Bw. Mathias Makanyaga atatupa karata yake kwenye Fainali ya mbio za mita 800.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.