Habari za Punde

Mysol Yazindua Huduma Zake Jijini Zanzibar

Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Shaibu Hassan Kaduara akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Duka jipya la vifaa vya umeme wa jua la Kampuni ya Maysol Engie liliopo Gulioni Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mysol , Godfrey Mugambi akizungumza katika ufunguzi wa duka jipya la vifaa vya umeme wa jua la kampuni hiyo liliopo Gulioni Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini magharibi, Idrissa Kitwana Mustafa akizungumza katika ufunguzi wa duka jipya la vifaa vya umeme wa jua la Kampuni ya Maysol Engie liliopo Gulioni Zanzibar.
Shamrashamra za uzinduzi wa Duka la Mysol Golioni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.

 MySol, kampuni inayoongoza nchini Tanzania kwa kuwezesha wateja kufanya malipo kwa awamu wakati huohuo wakipata huduma (PayGo)   katika tasnia ya nishati ya umeme wa jua na sehemu ya kampuni ya ENGIE Energy Access, zimetangaza na kuzindua ushirikiano wa shughuli zake za kibiashara Zanzibar.Uzinduzi huu ni moja ya mkakati wa kampuni wa kuboresha maisha ya watu milioni 20 hadi ifikapo mwaka 2025 kama kampuni inayoongoza kutoa huduma za nishati zinazobadilisha maisha, nafuu, zinazotegemewa na endelevu zenye kuleta uzoefu wa kipekee wa wateja kote (Tanzania Bara na visiwa vyake).

Katika hafla hiyo ya uzinduzi iliyowavutia wadau wa sekta hiyo, wakiwemo Viongozi wa Serikali, Wadhibiti wa Sekta ya Nishati, Viongozi wa Viwanda, Fedha, Ufundi, Washirika wa Usambazaji na Wadau wengine mbalimbali, Godfrey Mugambi, Mkurugenzi Mtendaji aliwaeleza waliohudhuria kuwa kampuni hiyo iko tayari, si tu. ili kuziba pengo la upatikanaji wa umeme nchini, lakini pia kuchangia kikamilifu katika upanuzi wa usambazaji wa umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme wa  gridi ya taifa.

"Tumepata mafanikio makubwa kwa kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya zaidi ya watu 750,000 kutoka kaya  zaidi ya 150,000 nchini kote upande wa Tanzania Bara. Upanuzi wetu kwa kuanza kutoa huduma Zanzibar ni sehemu ya mpango kabambe wa ukuaji wa ukuaji wa kasi zaidi na  nchini kote unaotuwezesha kuleta nishati yetu safi, ya uhakika na nafuu kwa mamilioni ya Watanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo”, Mugambi alisema.

Aliongeza kuwa kampuni ya MySol imedhamiria kutoa mchango wenye matokeo mazuri katika uchumi kwa kutoa suluhisho inayochangia maendeleo katika sekta muhimu za uchumi ikiwemo kilimo kupitia pampu za maji za umwagiliaji za jua kwa bei nafuu pamoja na umeme wa jua kwa matumizi ya viwandani.

Operesheni za kutoa huduma Zanzibar zimezinduliwa rasmi na Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mhe. Shahibu Hassan Kaduwara ambaye alipongeza hatua hiyo muhimu na kusisitiza kuwa uzinduzi wa biashara ya MySol unapaswa kwendana na juhudi za serikali katika kuongeza upatikanaji wa nishati. "Tunatarajia kuongezeka kwa uwezo wa kuleta suuluhisho na kumaliza changamoto ya ukosefu wa nishati katika maeneo ambayo hayajafikiwa nishati ya umeme wa gridi  ya taifa."

“Matarajio ya serikali ni kutoa huduma ya umeme kwa wote; kwa hivyo, hii ni fursa ya kutumia kutokana na mahitaji haya makubwa kusaidia kufanikisha malengo ya usambazaji wa umeme kwa kuendelea kuwekeza katika  jitihada za kufikisha umeme katika maeneo ambayo hajafikiwa na umeme .”

Waziri alipongeza mtindo wa ubunifu wa malipo kwa  awamu wakati ukiendelea kupata huduma (PayGo) unaosaidia kaya kwa kurahisisha malipo kupitia mifumo hii wakati huo wakiendelea kupata huduma ya mahitaji yao ya umeme. Alisema serikali pia inathamini mabadiliko chanya ambayo MySol italeta kwenye uchumi ikizingatiwa kuwa kuna ajira kadhaa za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja ambazo zitatengenezwa.

Kwa sasa, MySol inawekeza sana katika utengenezaji  wa nafasi za ajira na uwezeshaji wa ndani kupitia kutoa programu za mafunzo, bima ya afya, mipango ya kuweka akiba, na kuongeza fursa za ajira kwa kutoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi 150 wa kudumu, na zaidi ya mawakala 1,000  nawa wakandarasi wa kufunga huduma za umeme nchini kote nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.