Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzin Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Atowa Mkono wa Pole kwa Familia ya Mohammed Raza

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa Pole kwa Familia ya Marehemu Mohammed Raza aliyewahi kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja, na Mfanyabiashara Maarifu Zanzibar na Mwanasiasa, alipofika nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Hazrat Abbas  Jijini Dar es Salaam leo 9-6-2023, na (kulia kwa Rais) Mtoto wa Marehemu Hassan Mohammed Raza akiwa na wanafamilia
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mtoto wa Marehemu Mohammed Raza, Haasan Mohammed Raza (kulia kwa Rais)  alipofika nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Hazrat Abbas Jijini leo 9-6-2023, kwa ajili ya kutowa mkono wa pole kwa familia ya marehemu na (kulia kwake) Ndugu wa Marehemu Ibrahim Raza.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wanafamilia ya Marehemu Mohammed Raza, wakiitikia dua ya kumuombea marehemu, baada ya kutowa mkono wa pole kwa familia alipofika nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Hazrat Abbas Jijini Da es Salaam leo 9-6-2023. (kulia kwa Rais) Mtoto wa Marehemu Hassan Raza


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mtoto wa Marehemu Mohammed Raza,Hassan Raza baada ya kumaliza kutowa mkono wa pole kwa Familia ya marehemu alipofika nyumbani kwao Mtaa wa Hazrat Abbas Jijini Dar es Salaam leo 9-6-2023

 

1 comment:

  1. Makamu wa Rais wa Zanzibar, Usman Masood na Maulana Rajani walihudhuria mazishi ya mwanasiasa wa Zanzibar, Tanzania, katika nchi ya Afrika Mashariki, Muhammad Raza, usiku wa kuamkia leo.

    Zanzibar, Juni 9: Makamu wa Rais wa Zanzibar, Usman Masood na viongozi wengi wa kisiasa wa Zanzibar na Dar es Salaam mbali na Waafrika-Wahindi walihudhuria mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Uzini, Muhammad Raza, kiongozi wa kisiasa wa Khwaja Shia mwenye asili ya Kihindi kisiwani Zanzibar nchini Tanzania. , Afrika Mashariki Mbali na wasomi wa Kisunni wa Shia, Maulana Hasan Ali Rajani, rais wa Ligi ya Kitaifa ya India ya Kerala, chama cha kisiasa cha India, Mkoa wa Gujarat, alikuwa na ushiriki maalum. Viongozi wa kisiasa na kijamii wa nchi hiyo akiwemo Rais wa nchi hiyo Samia Hassan Sulawhi na makamu wa rais pia walifika kutembelea. Maulana Rajani Hassan Ali kutoka Dar es Salaam alielezea masikitiko yake na kusema kwamba huduma za marehemu Muhammad Raza kwa kurejesha demokrasia. haki za binadamu hazisahauliki Na kifo chake kina madhara makubwa sana kwa shirika la haki za binadamu. Mwishowe Maulana Rajani alimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu na kusema, “Ewe Mola mpe nafasi marehemu huyu katika rehema zake, na uwape subira waliofiwa. Akitoa salamu zake za rambirambi na pole kwa wafiwa na wanafamilia, Rajani alisema katika kipindi hiki cha majonzi pia tunashiriki majonzi yao.

    From Hasan Bhai. East Africa Tanznia Dar Es Salaam Cell No +255745344366 whatsaap +919998269850

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.