Na. Mwandishi Wetu Mwanza.
Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) limetoa zawadi ya Piki piki kwa wakala wake Sunshine Insurance Agency kama njia ya kuthamini mchango wake na jitihada alioonesha katika mwezi wa Aprili, 2023.
(ZIC)limemzawadia Piki piki aina ya TVS 125 wakala
wake aitwae Sunshine Insurance Agency katika kuthamini mchango mchango wake
katika ukuaji wa Biashara kwa Shirika hilo hususan kwa Mwezi Aprili, 2023.
Shirika la Bima la
Zanzibar (ZIC) linatarajia kuadhimisha miaka 54 katika biashara ya bima ifikapo
tarehe 20 ya mwezi Juni, 2023. Katika kuhakikisha wanaendelea kuwanyanyua
mawakala wao kwa kuwapatia vitendea kazi mbali mbali, Shirika limekuja na
mpango wa kutoa pikipiki kwa kila wakala ambae atafanya vizuri zaidi katika
kila mwezi.
Katika hafla ya
kukabidhi pikipiki hiyo kwa Sunshine Insurance Agency, Meneja wa Kanda ya Ziwa
Ndg. Bahatisha Suleiman amewapongeza washindi hao kwani jitihada zao binafsi ndiyo
zilizopelekea kushinda zawadi hiyo.
Kwa upande wake Afisa
Uhusiano wa Shirika la Bima la Zanzibar Ndg. Mohamed Shaaban amesema zawadi hii
itakwenda kuwa chachu ya jitihada kwa mawakala wengine ambao nao wana nafasi ya
kujishindia pikipiki katika miezi ijayo.
Aidha, Uongozi wa Sunshine Insurance Agency kupitia Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Ndg. Happiness Lyatuu Mkelemi wametoa shukurani zao za dhati kwa kupatiwa zawadi hiyo na wameahidi kuendelea kuwahudumia wateja wa Shirika la Bima la Zanzibar kama dira na mikakati ya Shirika hilo inavyoelekeza.
No comments:
Post a Comment