Habari za Punde

Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Yatia Fora Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akiwa kwenye kwenye banda la Wizara hiyo Juni 30, 2023 katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 47 (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akirusha mpira wa kikapu kwenye goli la mchezo huo kwenye banda la Wizara hiyo Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 47 (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam. 

Na Eleuteri Mangi, Dar es Salaam

Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu amesema tangu Rais wa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameingia madarakani amehamasisha masuala ya Utamaduni na Michezo ambaye inaendana na utamaduni wetu wa kitanzania.

Naibu Spika Mhe. Zungu amesema hayo Juni 30, 2023 mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 47 (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

“Kwanza tangu Mhe. Rais ameingia kwenye nafasi hii, amehamasisha sana masuala ya Utamaduni na Michezo, Tanzania tumevuka na tumeona vilabu vyetu hivi vikubwa vya Dar Young Africans na Simba Sports Club Kwenda mbali sana kwenye mashindano mbalimbali ya Afrika na hayo yote yanatokana na hamasa ya Mhe. Rais” amesema Naibu Spika.

Aidha, Naibu Spika Zungu ameipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya Waziri wake Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Katibu Mkuu wake Bw. Saidi Yakubu pamoja TanTrade kwa kazi nzuri ya maonesho ya 47 SabaSaba ambayo yamevuka mipaka na kushirikisha nchi mbalimbali duniani.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema Wizara yake imejikita kwenye maonesho haya kuwahudumia wadau wake katika sekta zote tatu za Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Banda la Wizara hiyo limekuwa kivutio kwa watu wengi kulitembelea na kupata burudani kedekede kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo Sholo Mwamba, msanii wa Singeli, kikundi cha ngoma cha Wane Star pamoja na kikundi cha Lumumba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.