Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akiwa ameongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mhe Jamal Kassim Ali na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Mbarouk Nassor Mbarouk (katikati) wakati wa kuingia kwenye Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mhe Jamal Kassim Ali (kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Mbarouk Nassor Mbarouk, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Mhe Jamal Kassim Ali (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto), na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akijadili jambo na Afisa Dawati wa SADC kutoka Wizara hiyo, Bw. Joseph Haule, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akifurahia jambo na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa (wa pili kulia), Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara hiyo, Bw. James Msina (kushoto) na Mhandisi Mkuu, Mafuta na Gesi, Wizara ya Nishati, Joyce Kisamo, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Luanda Angola.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Bw. James Msina (wa nne kulia) na Afisa Dawati wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wa Wizara hiyo, Bw. Joseph Haule (wa tatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania, pembezoni mwa Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC, jijini Luanda, Angola.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Luanda, Angola.
No comments:
Post a Comment