Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi aelekea Dodoma kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi ameondoka Zanzibar leo jioni na kuwasili Jijini Dodoma kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitakachofanyika kesho Chamwino, Dodoma.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein  Ali Mwinyi, leo Jumatano Tarehe 16 Ogasti, 2023, ameondaka Zanzibar kuelekea Dodoma kuhudhuria, kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM, Taifa

Rais Dk. Mwinyi ameambatana na Mama Mariam Mwinyi na ujumbe alioongozana nao wakiwemopm viongozi wa Chama Cha Mapinduzi.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Abeid Amani Karume, Rais Dk. Mwinyi aliagwa na viongozi mbalimbali  wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Ustafa pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama.

Uwanja wa ndege wa Dodoma, Rais Dk. Mwinyi alipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekiweri.

IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.