Habari za Punde

*Dkt. Chana Afungua Kikao cha Faragha cha Viongozi wa Wizara ya Utamaduni*

Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza na kikifungua Kikao cha Faragha cha Viongozi wa Wizara na Wakuu wa Taasisi za Wizara hiyo kilichofanyika Mkoani Morogoro.

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amefungua Kikao cha Faragha cha Viongozi wa Wizara na Wakuu wa Taasisi leo Agosti 16, 2023 mkoani Morogoro.
Mhe. Chana amesisitiza kuwa, vikao vya aina hiyo, vinatoa fursa ya kujitafakari kukumbushana namna ya kutekeleza majukumu ya Wizara na Taasisi ili kusaidia mabadiliko zaidi  katika nchi.
"Natambua kuwa majukumu ya wizara kwa mujibu wa muundo ni kuhudumia wadau wa sekta tunazozisimamia ili kuhakikisha kuwa matarajio ya Serikali ya Awamu ya Sita pamoja na ya wadau wetu yanafikiwa kwa kiwango kikubwa," amesema Mhe. Chana.
Awali Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema wizara hiyo inamgusa kila mtu katika kupata burudani, ajira, uhusiano na kipato, ambapo amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye ligi bora Duniani, Wanamuziki wengi  wanaounganishwa na lugha ya Kiswahili na kwa sasa  inakamilisha maboresho katika Sera ya Utamaduni ili iendane na wakati wa sasa, 
Aidha,  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima amesitiza muendelezo  wa  kuutangaza Utamaduni wa Taifa ili ujulikane kwa mila, desturi na utu wetu bila kusahau sekta yetu ya michezo ambayo inaendelea kukua siku hadi siku.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Saidi Yakubu amesema 
Mkutano huo ni Utekekezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa mwezi Machi, 2023 jijini Arusha wakati wa kikao cha faragha cha viongozi, na kitakua na  mada mbalimbali ikiwemo Vipaumbele na Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2023/24, pamoja na Mabadiliko ya Taasisi.
Kikao hicho kitafanyika kwa siku tatu kuanzia Agosti 16 hadi 18, 2023 ambacho kinahudhuriwa na  Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo, Wakuu wa Taasisi na Wakurugenzi Wasaidizi wa Wizara hiyo.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema wizara hiyo inamgusa kila mtu katika kupata burudani, ajira, uhusiano na kipato, ambapo amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye ligi bora Duniani, Wanamuziki wengi  wanaounganishwa na lugha ya Kiswahili na kwa sasa  inakamilisha maboresho katika Sera ya Utamaduni 





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.