Habari za Punde

Waziri Mhe.Jafo Azunguzia Kuhusu Biashara ya Kabini na Mikoko

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.

Serikali imesema itaendelea kuhamasisha upandaji wa mikoko katika maeneo ya pwani kwa ajili ya biashara ya kaboni na kusaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesema hayo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma leo Agosti 09, 2023.

Dkt. Jafo amesema kuwa ni kweli maeneo ya pwani yanapata changamoto ya kuliwa na maji ya bahari kutokana na kina kuongezeka hivyo Serikali inaendelea na jitihada za kukabiliana na changamoto hiyo kwa kujenga kuta na matuta kwa ajili ya kupunguza kasi ya mawimbi ya bahari.

Amesema katika Biashara ya Kaboni Serikali inawakaribisha wawekezaji kutumia fursa hiyo kwa kupanda mikoko katika maeneo hayo ya pwani yenye changamoto hizo za kimazingira.

Amesema kuwa katika baadhi ya maeneo ya pwani mikoko inachukuliwa na maji hivyo inasababisha kingo za bahari kumomonyoka hivyo maji huingia nchi kavu na kusababisha mafuruko.

Aidha, Waziri Jafo amewahimiza wakulima kuendelea kulima zao la korosho na kusema kuwa mbali ya kuwapatia faida wakati wa uvunaji pia watafaidika na biashara ya kaboni hivyo kuunga mkono juhudi za kupunguza hewa ya ukaa.

“Tutaendelea kutoa elimu kwa halmashauri nchini wapate utaratibu mzuri wa kuhusu kushiriki katika Biashara ya Kaboni kwani tayari tunashuhudia kule wilayani Tanganika wamenufaika,” amefafanua Dkt. Jafo.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakifuatilia kikao cha kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.

Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Ramadhan Suleiman Ramadhan akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Dustan Shimbo akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakati wa kikao cha kikao cha kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma
Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Ramadhan Suleiman Ramadhan akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma

                                  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.