Habari za Punde

Mhe Othman ashiriki Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Tawi la Masipa, Pandani Wilaya ya WeteMakamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, jana Jumatatu Septemba 18, 2023 ameshiriki katika Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Tawi la Masipa, huko Pandani Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, yeye akiwa ni Mjumbe.
Baada ya Kikao hicho, Mheshimiwa Othman amejumuika hapo, pamoja na Wajumbe Wenzake katika Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Jimbo la Pandani, pia Wilaya ya Wete Pemba.
Vikao hivyo, pamoja na mambo mengine, vimelenga kufanya Tathmini baada ya Zoezi lililoanza hivi karibuni la Uchaguzi wa Ndani ya Chama hicho, la kuwapata Viongozi Wapya, katika Ngazi zote za Uongozi.
Kitengo cha Habari,
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Septemba 18, 2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.