Habari za Punde

Mhe Othman ashiriki maziko ya Bi. Asha Ali ShaameMakamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, Leo Jumanne Novemba 14, 2023 amehudhuria pamoja na Waumini mbali mbali, katika Maziko ya Bi. Asha Ali Shaame.
Marehemu Bi Asha aliyefariki Dunia mapema usiku wa kuamkia leo Novemba 14, 2023 huko nyumbani kwake Jang'ombe, amesaliwa Masjid Hidaya, Mskiti uliopo hapo hapo Jang'ombe Mshelishelini na kuzikwa katika Makaburi ya Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini-Magharib, Unguja.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi, Amiin!
Innalillahi Waina Ilayhi Raajiun!
Kitengo cha Habari,
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Novemba 14, 2023.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.