Na.Mwandishi OMPR.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea kuhakikisha mipango ya Sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya Afya inafanikiwa kwa uweledi mkubwa kwa kusimamia huduma ziweze kuwafikia wanchini katika maeneo tofauti nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo katika Hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kwenye Mkutano Mkuu wa Nne (4) wa Chama Cha Wataalamu wa Viungo na Vifaa Tiba Saidizi (APOT) unakwenda sambaba na kilele cha siku ya Wataalamu wa Viungo na Vifaa Tiba saidizi Duniani uliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdul- Wakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya ina dhmana kubwa ya kusimamia masuala yanayohusu watu wenye ulemavu wa viungo, uhitaji wao na kuhakikisha huduma bora zinawafikia kwa ukaribu zaidi kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo wanaohusika na masuala ya watu wenye Ulemavu ili kuzidi kuimarisha upatikanaji wa huduma bora.
Rais Dkt. Mwinyi ameelza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetunaga Sera ya Taifa ya Maendeleo na huduma za watu wenye Ulemavu ya mwaka (2004 ) na sheria ya watu wenye Ulemavu ya (2010) kw alengo la kuhakikisha haki za watu wenye Ulemavu zinazingatiwa sambamba na kuimarisha miundombinu rafiki kwa ajili ya yao.
Amefahamisha kuwa sheria hiyo imeelekeza jinsi ambavyo watu wenye ulemavu watapewa kipaumbele kwenye masuala ya ajira, fursa na nafasi katika kupata huduma na kujumuika na jamii sambamba na kupinga unyanyasaji wa aina yoyote ile kwa watu wenye ulemavu.
Sambamba na hayo Mhe. Rais Dkt Mwinyi amesema katika kukabiliana na upungfu wa wataalamu wa kutoa huduma za viungo tiba na vifaa saidizi nchini Serikali kupitia Wizara ya Afya imeajiri wataalamu katika Hospital za Rufaa za Mikoa, Kanda, Hospital za Taifa na Hospital za Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Aidha Serikali imeandaa na kuzindua mpango mkakati wa huduma za utengamano na tiba shifaa ambao utaimarisha huduma za utengano hapa nchini na kuwataka watendaji wa Afya na wananchi kuusoma mpango huo na kutoa maoni na mapendekezo yatakayofanikisha utekelezaji mzuri wa mpango mkakati uliopitishwa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Mhe. Hassan Khamis Hafidh ameutaka Umoja wa Wataalamu wa Viungo na Vifaa Tiba saidizi kuhakikisha wanatoa fursa sawa kwa wanachama wote hasa katika masuala ya kujiendeleza kielimu na utowaji wa huduma bora .
Mhe. Hassan amesema katika upatikanaji wa ajira Tanzania watu wenye ulemavu wamepewa kipao mbele na nafasi maalumu katika masuali ya ajira na kuwataka kuomba ajira hizo zinapotangaziwa .
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Tanzania Bara Ndugu Omar Kibuyu amewataka wanataaluma kutanua wigo katika kufanya kazi za kuwasaidia wenye uhitaji wa Vifaa Tiba saidizi sambamba na kujiendeleza katika taaluma hiyo ili kupunguza changomoto ya uhaba wa wataalamu wa kutengeneza na kutoa matibabu ya Vifaa Tiba saidizi hapa nchini.
Nae Raisi wa chama cha Wataalamu wa Viungo na Vifaa Tiba Tanzania Ndg. EXAUD YUSTO KASEGEZYA amesema chama hicho kimefanikiwa kuanzisha kwa upatikanaji wa vifaa Tiba katika hospital ya Mnazi Mmoja na Chake Chake Pemba pamoja na kuwapatia ufadhili wa masomo kwa wataalamu wanaojiendeleza na shahada ya pili katika kada hiyo.
Amesema licha ya mafanikio hayo lakini chama hicho kinakabiliwa na changomoto mbali mbali ikiwemo kutokuwepo kwa Kurugenzi ya huduma ya utengamano katika ngazi ya Wizara, Hospital za Mkoa na Wilaya jambo ambalo linazorotesha upatikanaji wa huduma bora ya Tiba ya Viugo na Vifaa saidizi.
Aidha Ngugu Exaud amefahamisha kuwa ushirikishwaji wa wataalamu wa Viungo na Tiba saidizi katika ngazi za maamuzi umekuwa mdogo na baadhi ya wakati kutokushirikishwa kabisa jambo ambalo linapelekea kutopatikana kwa mchango sahihi katika ngazi za maamuzi .
Aidha wameiomba Serikali huduma za Viungo na vifaa Tiba saidizi kuwekwa katika Mfuko wa Bima ya Afya ili kuwawezesha wananchi hasa wenye Ulemavu kuweza kumudu upatikanaji wa matibabu sambamba na kendelezwa kwa wataalamu wa Sayansi ya Viungo Tiba saidizi kwa ngazi ya Shahada ya kwanza na ya Tatu ili kuongeza nguvu wa utowaji wa huduma hizo nchini.
Mpema Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla alikagua mabanda ya maonesho na kupata maelezo juu ya Taaluma ya Viungo na Vifaa Tiba Saidizi yenye mnasaba na Maadhimisho hayo.
Imetolewa na kitengo caha Habari (OMPR)
LEO Tarehe 05.11.2023
No comments:
Post a Comment