Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Amemuwakilisha Rais wa Zanzibar Mhe Dk.Hussein Mwinyi Katika Matembezi ya UVCCM na Miaka 60 ya Mapinduzi Matikufu ya Zanzibar



Makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussen Ali Mwinyi amesema Serikali zote Mbili  zitaendela kuwaweka mazingira mazuri kwa Vijana ikiwemo kuwapatia Elimu, Mikopo na fursa mbali mbali mbali ili kuweza  kufikia malengo waliojiwekea.

Ameyasema hayo katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mjumbe wa kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla katika uzinduzi wa Matembezi ya Umoja wa Vijana yenya Mnasaba na Sherehe za kutimia miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba.

Amesema Matembezi  haya yanaendana na fikra na falsafa za waasisi wa Mapinduzi hivyo ni lazima Vijana kuyatumia matembezi haya katika  kuyatangaza mambo mazuri yanayofanywa na viongozi wakuu wa nchi ambayo ni kuwaletea maendeleo wananchi wake bila ya kubagua Dini, Rangi wala Itikadi ya chama chochote.

Rais Dkt. Mwinyi amesema mapinduzi ya mwaka 1964 yaliyofanywa na viongozi waliopita yalikuwa na lengo la kuwakomboa wananchi kutoka katika mikono ya wakoloni hivyo ni lazima vijana kwa kushirikiana na viongozi wa serikali zote mbili kuyaenzi kwa vitendo katika kuwaletea maendeleo wananchi wake na kuwaondolea changamoto zote zinazowakabili.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa wajibu wa Vijana ni kulisaidia Taifa katika kupiga vita Rushwa, ubadhirifu wa mali za Umma, Udhalilishaji na Madawa ya kulevya kwa kuwapa Elimu vijana wenzao ili Taifa liweze kusonga mbele  pamoja na kuweza  kutoa ushirikiano kwa vyombo husika ili kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria wwale wote wanaoenda kinyume na sheria.

Sambamba na hayo amewataka Viongozi wa matembezi hayo na Vijana kwa ujumla kusimamia nidhamu ili kufikia lengo la kuwepo kwa jumuiya hio  kwani Jumuiya ya  Vijana  ndio Tegemeo kubwa la  Chama na Taifa kwa Ujumla  katika kupata viongozi bora wa sasa na baadae.

Akizungumzia Uandikishaji wa daftari la kudumu la Wapiga Kura  Rais Dkt. Mwinyi amewataka vijana wenye sifa kujitokeza kujiandikisha  ili wapate nafasi ya kukichagua Chama Cha Mapinduzi kwa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020-2025.

Nae Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ndugu Mohamed Ali  Mohamed (KAWAIDA ) amesema ndani ya Miaka 60 ya Mapinduzi, Zanzibar imepiga hatua kubwa ya maendeleo ambapo Serikali ya Awamu ya nane(8) na serikali ya awamu ya Sita (6) zinaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya kimaendeleo kwa  kujenga miradi mbali mbali pamoja na kuwaodolea changamoto zote wananchi wake.

Ndugu Mohammed Kawaida amefahamisha kuwa matembezi ya vijana yana azma ya kuyalinda na kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambapo kupitia matembezi hayo vijana watafanya kazi ya kuyatangaza yale mambo makubwa na mazuri yaliyofanywa na Viongozi wakuu wa Nchi yenye tija na wananchi wa Tifa hili.

Amesema kuwa dhamira ya Mapinduzi ni kuwaletea wananchi maendeleo na kuwapa nafasi Vijana kuweza kujitawala wenyewe hivyo Jumuia ya Umoja wa Vijana itaendelea kukitumikia chama cha Mapinduzi na kuwalinda viongozi wakuu wa nchi kwa kuhakikisha wanawaweka tena madarakani ifikapo mwaka 2025.

Akizungmza kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Katibu wa CCM Idara ya Itikadi na Uwenezi na Mafunzo ya CCM Zanzibar Comred Khamis Mbeto amesema kuwa wajibu wa Vijana ni kuyalinda Mapinduzi kwa kuzienzi na kuzidumisha falsafa na fikra za waasisi wa mapinduzi ambao walijotoa kwa ajili ya wazanzibari.

Amesema kuwa Vijana ndio hazina ya Chama cha Mapinduzi ambao wana mchango mkubwa katika kuhakikisha wanapambania maendeleo ya Nchi na kutokuwapa nafasi ya kuwapotosha Vijana wale wote ambao hawana dhamira njema na CCM na Serikali kwa ujumla.

Maapema mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba  Mhe. Matar Zahor Maoud amesema kuwa kupitia mapinduzi matukufu ya Mwaka 1964 Zanzibar tumepata maendeleo makubwa ambayo yanaletwa na viongozi wakuu waliopo sasa na waliopita hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuyapigania na kuyaenzi maendeleo hayo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.

Amesema Zanzibar inaendelea kunufaika na matunda ya Mapinduzi kwa kupitia viongozi wakuu wa nchi hivyo amewashukuru viongozi wakuu wa nchi kwa kuwaletea miradi mingi ya kimaendeleo ikiwemo maji safi na salama, Afya, ujenzi wa Skuli za ghorofa pamoja na kutatua changamoto zote zinazowakabili wananchi wa mkoa wa kusini pemba na mikoa mengine.

Imetolewa na kitengo Cha Habari (OMPR)

Leo tarehe….28.12.2023

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.