RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kumjulia hali yake Msanii Maarufu
wa Zanzibar Bi.Mwapombe Hiyari, alipofika nyumbani kwake Chuini Wilaya ya
Magharibi “A” Unguja leo 23-2-2024, ikiwa ni utaratibu wake kuwajulia hali
Wazee mbalimbali Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Familia ya Mzee Daudi
Suleiman Ali, , kuitikia dua, alipofika nyumbani kwake Fuoni Wilaya ya
Magharibi “B” Unguja kwa ajili ya kumsalimia na kumjulia hali yake leo
23-2-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Mzee Ramadhan
Nzori , aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Jangombe Zanzibar, alipofika nyumbani
kwake Jangombe Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya mazungumzo na kumjulia hali
yake leo 23-2-2024
No comments:
Post a Comment