Habari za Punde

MKUTANO MKUU WA BARAZA UWT MKOA WA MJINI KICHAMA

Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Kichama Inocent Nanzabar wakati akifungua Baraza la UWT Mkoa wa Mjini Kichama, uliofanyika Matarumbeta Wilaya Mjini.

Na Takdir Ali. Maelezo. 10.03.2024.

Viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini kichama wameahidi kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo ili kuwaondoshea usumbufu Wananchi katika maeneo yao.

Hayo yameelezwa na Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mjini kichama Mhe. Fakharia Shomari Khamis na Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa huo Mhe. Saada Ramadhan Mwendwa huko katika Tawi la CCM Matarumbeta wakati walipokuwa wakitoa maelezo katika Baraza kuu la UWT Mkoa wa Mjini.

Wamesema kwa kipindi cha mwaka mmoja, Januari hadi Desembar 2023 wameweza kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi katika masuala mbalimbali ikiwemo ya Wanawake, Watoto Mayatima, Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na Ujasiriamali.

Aidha wamesema Viongozi wakuu wa kitaifa Mhe. Dkt. Samia Suluh Hassan na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wamevuuka malengo katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi hivyo amewaomba kuwaunga mkono ili wazidi kutekeleza majukumu yao na kufanya kazi kwa Ufanisi.

Kwa upande wake Katibu wa UWT Mkoa wa Mjini kichama Maryam Iddi Kireti amewataka Wanawake wenzao kuwa na uthubutu, Uimara na kujiamini ili kuweza kufanya ushawishi wa kimaendeleo katika maeneo yao.

Aidha amewapongeza UWT katika Mkoa huo kwa kufanya kazi nzuri katika Uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura na kuweza kupata idadi kubwa ya Wanawake katika Daftari hilo na kuwaomba kushajiisha wenzao kujitokeza kwa wingi wakati litakaporudi kwa awamu ya pili.

Mapema akifungua Baraza hilo Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini kichama innocent Nazebari amewakumbusha Wabunge, Wawakilishi na Madiwani katika Mkoa huo kushuka chini kwa Wananchi na kuwasemea mambo mazuri yanayofanywa na Viongozi wao wa kitaifa ili jamii kuzidi kujenga na Chama hicho.

Hata hivyo amewataka kufanya Vikao vya mara kwa mara ili kuweza kubaini matatizo yanayowakabili wanawake wenzao na kuyatafutia ufumbuzi wa haraka.

Mwenyekiti UWT Mkoa wa Mjini Kichama Ghanima Sheha Mbwara  akimkaribisha mgeni rasmi Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Kichama Inocent Nanzabar kufungua mkutano wa Baraza la UWT Mkoa wa Mjini Kichama, huko Matarumbeta Wialaya ya Mjini.

Mjumbe wa Baraza kuu la UWT Mkoa wa Mjini Kichama ambae pia ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Mgeni Hassan Juma akichangia katika Mkutano wa Baraza hilo, uliofanyika katika tawi la Matarumbeta Wilaya ya Mjini.Mjumbe wa Baraza la UWT Mkoa wa Mjini Kichama ambae pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini kichama Mhe. Fakharia Shomari Khamis akichangia katika Mkutano Baraza hilo, uliofanyika Matarumbeta Wilaya ya Mjini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.