Habari za Punde

MAADHIMISHO YA WIKI YA KUWAKUMBUKA VIONGOZI YAENDELEA

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya  Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban akiongoza familia ya   Marehemu Khafidh Suleiman Almas  kumuombea dua   mzee huyo katika wiki ya kuwakumbuka waasisi waliotangulia mbele ya haki inayoanzia April 01-7, hafla iliyofanyika  huko Kinduni Kichungwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Na Ali Issa. Maelezo Zanzibar .

Waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaban amesema Serikali itaendelea na utaratibu wa kuwaombea Dua marehemu walioitumikia nchi kutokana na uzalendo na imani kubwa walioionyesha.

 

Ameyasema hayo wakati wa Dua ya kumuombea Dua wa Mapinduzi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 marehemu Hafidhi Suleiman Almas, iliofanyika Kinduni Mkoa wa Kaskazini Unguja.

 

Amesema kuwaombea Dua waasisi ni jambo la msingi kwani mtu akishakufa kinachofuata ni kuombewa Dua kwa Mwenyezi Mungu na wajibu wa binaadamu.

 

Aidha amesema mchango aliotoa marehemu hautoweza kusaulika daima kwani mchango wake ndio ulioifanya nchi kuwa huru.

 

Amefahamisha kuwa ni vyema kuyaenzi yale yote mema walioachiwa ambayo ni utu, heshima, ubinaadamu na kuishi kwa kupendana na kuhurumiana.

 

Nae mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Rashid Hadid Rashid amesema kuwa Dua hiyo ni utaratibu unaoendelea kuyaenzi na kukuza Uzalendo na kuitumikia nchi kwa upendo na heshima.

 

Aidha amesema Serikali itaendelea kuwakumbuka na kuwathamini marehemu hao kutokana na mchango wao walioutowa wakati wa uhai wao.

 

Kwa upande wake Naibu Kadhi wa Wilaya ya Kaskazini ‘‘B’’ Sheikh Abubakar Ali Muhamed akiongoza Dua hiyo iliowajumuisha familia ya muasisi huyo amesema kuwa Dua ni jambo jema kuwaombea watu waliotangulia mbele ya haki.

 

Hata hivyo amefahaisha kuwa ni jambo jema na linapaswa kuendelea na kumuombea mja msamaha kwa mola wake.

 

Nae Idd Hafidhi Suleiman akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Familia hiyo ameishukuru Serikali kwa kuona kuwa Mzee wao bado anajaliwa na kumthamiwa jambo ambalo ni jema na linapaswa liendelee kumkumbukwa na kumuombea Dua kwa Mwenyezi.

 

Marehemu Hafidh Suleiman Almas ambae ni miongoni mwa waasisi wa Mapinzuzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 alizaliwa mwaka 1939 na kufariki mwaka 1989 na kuzikwa kinduni kichungwa Wilaya ya Kaskazini ‘‘B’’.

Sehemu ya familia ya Marehemu  Mzee Khafidh Suleiman Almas wakiwa katika dua maalum ya kumuombea mzee huyo ikiwa ni muendelezo wa wiki ya kuwakumbuka waasisi waliotangulia mbele ya haki  inayoanzia April 01-7, hafla iliyofanyika  Kinduni Kichungwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Waziri wa Biashara na maendeleo ya  Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban akimkabidhi kiongozi wa familia Iddi Khafidh Suleiman ubani kwa niaba ya serikali mara baada ya kumuombea  Marehemu  Khafidh Suleiman Almas ikiwa ni kutambua mchango wa mzee huyo ,katika muendelezo wa ziara kutembelea makaburi ya  viongozi waliotangulia mbele ya haki,hafla iliyofanyika  huko Kinduni Kichungwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya  Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban akizungumza na  familia ya Marehemu Khafidh Suleiman Almas, baada ya   kumaliza kumuombea dua  mzee huyo katika wiki ya kuwakumbuka waasisi waliotangulia mbele ya haki inayoanzia April 01-7, hafla iliyofanyika  huko Kinduni Kichungwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Rashid Hadid Rashid  akimkaribisha Waziri wa Biashara na maendeleo ya  Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban kutoa nasaha kwa familia ya Marehemu  Khafidh Suleiman Almas  mara baada ya kumuombea dua mzee huyo katika maadhimisho ya wiki ya kuwakumbuka waasisi hao inayoanzia April 01 -7, hafla iliyofanyika Kinduni Kichungwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.