Habari za Punde

SEKTA YA UHIFADHI NA MALIASI IMEKUA NA MCHANGO KWA HALAMSHAURI AWASHUKURU USAID KUPITIA MRADI“TUHIFADHI MALIASILI” KUENDELEA KUSAIDIA

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara Anna Mbogo, akizungumza na waandishi wa habari za Mazingira Tanzania wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya hifadhi ya malia Alisi, ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, unaotekelezwa na JET.

                                  Picha na Abdi Suleiman -BABATI 

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara Anna Mbogo, akizungumza na waandishi wa habari za Mazingira Tanzania wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya hifadhi ya malia Alisi, ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, unaotekelezwa na JET.


Na. Abdi Suleiman -- BABATI.

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara Anna Mbogo, amesema kuwa sekta ya uhifadhi wa maliasili imekua na mchango mkubwa ndani ya halmashauri hiyo pamoja na vijiji vilivyozungukwa na maliasili hizo.

Aliyataja maeneo ya hifadhi ya Maliasili hizo ni Tarangire, Hifadhi ya Jamii Burunge, ziwa Burunge na ziwa Manyara huku Vijiji 10 vikiunda hifadhi ya Jamii Burunge.

Mkurugenzi huyo aliyaeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa Mazingira Tanzania (JET), wakati wa ziara ya kutembelea maeneo  mbalimbali ya hifadhi, ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili unaotekelezwa na JET.

Alisema vijiji hivyo vilitoa maeneo yao kwa ajili kutenga eneo lililowezesha kuwepo hifadhi hiyo ya jamii, na kwa uwepo wa hifadhi hiyo kumewezesha kuwepo kwa mafanikio mengi kwani wanapata watalii kuja kuangalia wanyama, kupumzika na kwa ajili ya utalii wa Picha.

“Kijiji kama Sangaiwe kina hifadhi yake pekee hapa wananchi wananufaika na utalii wa picha na utalii wa Wanyama, hii yote ni kutokana na umuhimu wa uhifadhi tulionao,”alisema.

Aidha alisema Halmashauri kwa mwaka inapata mapato yanayofikia kiasi cha shilingi Milioni 300 kutokana na Utalii, fedha hizo zinakuja kwa awamu, kwa upande wa vijiji vyote 10 mapato yao yanafikia Bilioni mbili kutoka WMA, na Kijiji kimoja kinauwezo wakupata Zaidi ya Milioni 600 akitolea mfano wa Kijiji cha Sangaiwe.

“Katika kipato kinachopatikana katika maeneo ya hifadhi ya jamii kupitia TAWA tunapata 15% nje ya WMA kinapelekwa halmashauri, na eneo la WMA pia asilimia 10% inaingia halmashauri, fedha hizo tunakua na uwezo wa kufanya maendeleo katika maeneo yaliyomo ndani ya halmashauri kwani inavijiji 102 na kata 25,” alisema.

Alifahamisha kwamba kijiji cha Sangaiwe kinauwekezaji nje ya WMA kinaweza kupata milioni 600 au 800 kupitia utalii, hata bajeti yao wakijumuisha na wanazopata kutoka WMA wanaweza kupata hata bilioni na kufanya maendeleo mkubwa.

“Angalia Kijiji cha Sangaiwe wameweza kujenga madarasa, kujenga shule mpya Burunge kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea, na sasa wanajenga nyingine, wamejenga hopitali, Ofisi ya Kijiji, yote hiyo ni kupitia mapato ya wanayoyapata kutokana na uhifadhi,”alifahamisha.

Aidha alisema vijiji vingine kama kata ya Nkaiti, wamejenga shule ya sekondari mpya baada ya iliyokuwepo awali, eneo la Mdori wamejenga sekondari ya Burunge, kijiji cha Kakoi kipo hifadhi ya Tarangire nao wanajenga sekondari kwavile wanafunzi wapo katika mazingira hatarishi wanawapunguzia umbali wa kutembea kupita kwenye Wanyama.

Hata hivyo alisema halmashauri inajivunia kuwa na hifadhi hizo, ndio maana wanahamasisha wananchi kuendelea kutunza mazingira, na wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi, Serikali za vijiji kwamba wafanye shughuli zao zinazoendana na maliasili, kwa kuona shughuli zipi rafiki na zipi sio rafiki.

Alisema iwapo Shoroba ya Kwakuchinja inayounganisha Hifadhi ya Tarangire na Manyara, kama ikizibwa wanyama hawatakua na uwezo wa kuvuka kutoka Tarangire kwenda Manyara, Ngorongoro, Serengeti, hivyo wananchi waendelee na shughuli zao za kibinaadamu zile rafiki kwa uhifadhi wa mazingira.

Alisema wadau wengi wamehamasisha kuwawezesha akinamama kupitia vikoba, kusuka mikeka, kuweka akiba, shughuli za biashara zote ni jitihada za kuhifadhi maliasili.

Hata hivyo alisema watahakikisha hifadhi za Tarangire, Burunge WMA, Manyara, zinawaletea manufaa zaidi wananchi na serikali iweze kupata kipato, kwani iwapo Wanyama watatoweka hakuna watalii watakaokuja, serikali, wananchi na vijiji vyote vitakosa mapato.

“Kupitia hifadhi hizo faida nyingi zimepatikana ofisi zimeweza kujiendesha zenyewe, bila ya kufanya wananchi kuchangia, vijiji vinajitegemea vyenyewe,”alisema.

Aidha Mkurugenzi huyo aliwashukuru wadau wakiwemo USAID, Chem Chem na TNRF ambao wamejitosa katika kufanya shughuli za kuongoa Shoroba ya Kwakuchinja na kuahidi kuendelea kusaidiana watafanya mambo mengi makubwa.

MWISHO

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.