Habari za Punde

WAZIRI JAFO AKAGUA MAENDELEO UJENZI JENGO LA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la utawala la Ofisi ya Makamu wa Rais unaoendelea katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 02 Julai, 2024. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza mtaalamu wa ujenzi alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la utawala la Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 02 Julai, 2024. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la utawala la Ofisi ya Makamu wa Rais unaondelea katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 02 Julai, 2024.

Pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali ya jengo hilo, pia amekagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi) kinachojengwa katika jengo hilo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Waziri Jafo amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi ambaye ni Kampuni ya SUMA JKT kuongeza kasi katika ujenzi ili likamilike kwa wakati.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi akimuelezea Waziri amesema makavazi hayo yakuwa katika namna mbalimbali zikiwemo kwa mfumo wa elektroniki na nyaraka ngumu.

Hivyo, jingo hilo litakapokamilika pamoja na kuwawezesha watumishi kufanya kazi kwa ufanisi lakini pia kitasaidia kuhifadhi kumbukumbuku muhimu za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa vizazi vyote.

Aidha, katika ziara Mhe. Dkt. Jafo aliambatana na baadhi ya wakurugenzi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.