Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa
Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi aliyeambatana na ujumbe
wake Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na
Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusiana na Ziara ya Kiserikali
ya Mgeni wake Rais
wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi
Rais
wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akizungumza na Waandishi wa
Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusiana na Ziara yake ya Kiserikali nchini
Tanzania
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Msumbiji
Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakati wakishuhudia utiaji saini Hati ya Makubaliano
ya kushirikiana katika masuala ya Afya baina ya Tanzania na Msumbiji Ikulu
Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024. Kulia ni Waziri wa Afya Mhe. Ummy
Mwalimu akitia saini Hati hiyo kwa upande wa Tanzania na kushoto ni Naibu wa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Msumbiji Mhe. Manuel José Gonçalves
akitia saini kwa niaba ya Serikali.
No comments:
Post a Comment