Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Amekutana na Waziri wa Nishati wa Qatar

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi leo katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini Qatar .

Mapema asubuhi alikutana na Waziri wa nchi wa Qatar anayeshughulikia masuala ya Nishati Mheshimiwa  Saad bin Sherida Al- Kaabi.

Mazungumzo hayo yametoa nuru kwa Qatar kuiuzia Tanzania mbolea aina ya Urea kwa gharama nafuu.

Mazungumzo hayo alihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Qatar Mheshimiwa Habib Awesi Mohammed pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea ( TFC ) Samwel Ahadi Mshote. 

Kesho akimaliza ziara yake nchini Qatar Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kushiriki mkutano mkubwa wa Kimataifa wa  kutimiza miaka 30 ya Familia Duniani utakaofanyika jijini Doha.

Halikadhalika Mkutano huo unafuatia Azimio la mwaka 1994 la Umoja wa Mataifa la Mwaka wa Kimataifa wa Familia ( IYF ) lililopitishwa rasmi na Baraza la Umoja wa Mataifa likizingatia thamani na umuhimu uliopo wa kuzilinda na kuzisaidia familia kupitia sheria za Kimataifa.

Vilevile maazimio ya mwaka wa Kimataifa wa Familia hufanyika kila baada ya miaka kumi.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.