RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amebainisha mikakati ya Serikali juu ya ukuaji uchumi wa
Zanzibar na kueleza kuwa inaendelea kuwawekea mazingira rafiki ya biashara wafanyabiashara
wote wanaotumia bandari ya Zanzibar.
Dk. Mwinyi amesema hayo
alipozindua, kusaini na kushuhudia utiwaji wa saini Mpango wa maboresho ya utoaji
huduma kwa bandari ya Zanzibar (Zanzibar Port Improvement Charter) kwa
ushirikiano wa Serikali, wadu wa bandari kutoka taasisi za umma na binafsi
pamoja na Taasisi ya Tony Blair (TBI), hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu, Zanzibar.
Amesema, lengo la mpango huo ni
kuondosha usumbufu
kwa kupeana majukumu kwa kila mdau, kupitia viashiria vilivyoandaliwa ndani ya
mpango huo sambamba na kurahisisha ushushaji wa makontena (Makasha), ukaaji wa meli ukutani,
kusubiria ukuta pamoja masuala ya ‘Customes Clearance’ kwa kuongeza ufanisi wa utoaji
wa huduma za bandari ili kutoa msukumo wa ukuaji wa Uchumi wa nchi.
Akizungumzia
suala la upakiaji na ushushaji wa Makontena bandarini, Rais Dk. Mwinyi
amewahakikishia wafanyabiasha wa Zanzibar kwamba Serikali imedhamiria kwa dhati
kuimarisha utoaji wa huduma kwa kurahisisha mchakato wa upakiaji na ushushaji
wa kontena (Makasha) katika Bandari zote nchini.
Alisema, hatua hiyo ni kwa
mujibu wa wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020 hadi 2025 katika
Ibara ya 167(b) inayozungumzia Kuimarisha huduma za bandari kwa kutumia vifaa
na teknolojia za kisasa ili kuongeza idadi ya makontena (TEUs) kutoka 82,312
mwaka 2018 hadi makontena 105,000 ifikapo 2025 pia kupunguza idadi ya siku za
kuegesha meli kutoka siku saba mwaka 2018 hadi siku tano mwaka 2025 ambayo kwa sasa
uwezo wa bandari za makasha tatu;
Malindi, Fumba na Mkoani Pemba zina uwezo wa kuhudumia makasha zaidi ya
105,000.
Aidha Rais Dk. Mwinyi ameeleza
kuwa makubalianao hayo baina ya Serikali na taasisi hizo ni utekelezaji na
ufanisi kwa Babdari ya Zanzibar pia kutafanyika upimaji wa kila kilichotekelezwa
na taasisi hizo kila inapotimia mwaka mmoja.
Alitanabahisha
kwamba endapo taasisi zote zitatekeleza wajibu wao ipasavyo, mafanikio makubwa
yatapatikana nchini, akitolea mfano nchi za Singapore, Mombasa - Kenya, Gambia
kwa kufanikiwa na mpango kama huo wa utoaji huduma wa bandari ambao wamepiga
hatua kubwa ya mafanikio.
Katika hatua
nyengine ya kuboresha huduma za bandari Rais Dk. Mwinyi amesema, Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa Bandari
jumuishi ya Mangapwani inayotarajiwa kuhudumia meli kubwa za mafuta na gesi.
Alieleza ujenzi wa bandari hiyo unakwenda sambasamba na ilani ya Chama cha Mapinduzi
CCM, kifungu 167(c) kinachoielekeza
Serikali kujenga miundombinu ya
kuhudumia meli zinazopita mwambao wa Afrika Mashariki, kupata huduma za kuongeza
mafuta, maji safi na kufanya matengenezo.
Hata hivyo, Dk. Mwinyi
aliwataka wadau wa bandari ya Zanzibar ikiwemo Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Uchukuzi yenye kubeba jukumu kubwa la Taifa, la kusimamia miundombinu nchini,
kuendelea kuwa karibu na watumiaji wa miundombinu hiyo kwa kuwapelekea huduma
na nyenzo ili kuhakikisha wananchi wanatumia miundombinu bora na yenye tija kwa
ustawi wa jamii na kuinua uchumi wa Zanzibar kwa maendeleo ya wananchi.
Vile vile, Rais Dk. Mwinyi ameeleza
jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuongeza kasi ya ukuaji wa
uchumi wa nchi
wanashirikiana na wadau mbalimbali kuendeleza sekta ya Uchukuzi.
Akibainisha miongoni mwa
harakati hizo ni kuimarisha miundombinu ya barabara pamoja na bandari kwa Unguja
na Pemba ili
kuwarahisishia huduma wanachi na wafanyabiashara.
Pia, aliwaomba wafanyabiashara
waendelee kufanya kazi zao kwa uaminifu, maadili na uzalendo ili kujipatia
kipato halali na kuzingatia wajibu wao wa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria.
Akizungungumza kwenye hafla
hiyo, Waziri Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk.
Khalid Salum Mohamed amesema kusainiwa kwa Mpango huo wa maboresho ya utoaji wa
huduma za Bandari ya Zanzibar ni makubaliano baina ya Serikali na wadau wa
bandari hiyo zikiwemo taasisi za Umma na binafsi kufanyakazi kwa pamoja ili
kuongeza ufanisi na kuleta tija katika kukuza Uchumi wa nchi.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari, Akif Ali Khamis amepongeza
hatua ya Serikali kuleta Mapinduzi makubwa kwa sekta ya bandari ya Zanzibar juu
ya uendeshaji wa bandari hiyo baada ya kuingia mkataba na Kampuni za Zanzibar
Multiple, kampuni ya Bandari ya Fumba na ya Mkoani kwaajili ya kushusia makasha
(makontena.
Alisema, tokea kuanza maboresho yaliyosimamiwa na Kampuni ya Zanzibar
Multiple amesifu mafanikio makubwa yalitofikiwa na bandari hiyo ikiwemo
kupungua siku za kusubiri meli kutoka siku 40 hadi 20 hadi kufikia siku nane
kwa mara ya kwanza kutokea kwa bandari hiyo akisifu ufanisi wa kuhudumia meli
kuongezeka. Pia ametoa wito kwa wadau wa huduma badari hiyo, wabadilike na
hatimae waendane na ushindani wa bandari uliopo hivi sasa ulimwenguni.
Kwa upande wake kiongozi wa timu ya Taasisi ya Tony Blair, Frank Matsaert
amesifu juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuusimamia hadi
kuufanikisha mpango huo na kueleza kwamba utakwenda kufungua mafanikio ya
ukuaji wa Uchumi wa Zanzibar kupitia lango la Bandari hiyo.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU
ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment