Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amejumuika na Viongozi wa Serikali, Dini na Wananchi katika Swala na Maiti kumsalia aliyekuwa Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu, Marehemu Abdalla Ali Abdalla ( KITOLE ) iliyofanyika katika Masjid Nnabawy Mombasa baada ya Sala ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwao Uzini Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Inna lilah wainna ilayhi rajiun.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR).
Tarehe 06.12.2024
No comments:
Post a Comment