Tanzania na Vietnam zimekubaliana kuanzisha ushirikiano wa sekta binafsi ili kuchagiza kasi ya ukuaji wa biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.
Makubaliano hayo yamefikiwa kwenye mazungumzo yaliyofanyika leo Aprili 29,2025 kati ujumbe wa Tanzania na Vietnam uliojumuisha wafanyabishara na viongozi wa sekta binafsi kutoka pande zote mbili yaliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Chemba ya Biashara na Viwanda ya Vietnam jijini Hanoi.
Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo hayo umeongozwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Kombo.
Katika mkutano huo Wafanyabiashara wa pande zote mbili wamepata nafasi ya kushirikishana uzoefu wao na fursa za biashara na uwekezaji zilizopo na kupanga mikakati ya pamoja ya namna ya kutumia fursa hizo kwa manufaa ya pande zote mbili.
Miongoni mwa fursa zilizopata mwitikio mkubwa zaidi miongoni mwa wafanyabishara hao ni pamoja na zao la mkonge, vifaa vya ujenzi, uchumi wa buluu, madini hadimu, korosho na uwekezaji katika sekta ya kilimo.
Akizungumza katika mkutano huo Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bw. Vicent Minja amezisisitiza sekta binafsi kuchangamkia fursa zilizopo na zitakazo ibuliwa kwa manufa ya pande zote mbili.
Aliongeza kusema kuwa Serikali za pande zote mbili zimeonyesha utayari kwa kutengeneza mazingira mazuri ya biashara na zimekuwa zikitoa ushirikiano mzuri kwa wafanyabiashara hivyo ni vyema sekta binafsi ikatumia fursa hiyo kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kibiashara miongoni mwao ili kufikia malengo yanayokusudiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti na Rais wa Chemba ya Biashara na Viwanda ya Vietnam (VCCI) Bw. Pham Tan Cong ambaye pia alikuwa akiongoza ujumbe wa wafanyabiashara kutoka sekta mbalimbali, ameeleza utayari na shauku walioyonayo kufanya biashara na kuwekeza nchini Tanzania.
Aidha, ametoa rai kwa pande zote mbili kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa hapo awali, ikiwemo utekelezaji hati za makubaliano ya ushirikiano zilikwisha sainiwa.
Vilevile, Bw. Pham Tan Cong amependekeza kuanzishwa kwa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Vietnam litakalowawezesha wafanyabiashara kuongeza ushirikiano na uhusiano, pia kujadili na kushirikishana masuala mbalimbali ilikuongeza kasi ya biashara na uwekezaji kati ya pande hizo mbili.
Kwa upande wake Waziri Kombo amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi imara wa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango na nafasi ya sekta binafsi kwenye maendeleo ya Taifa hivyo itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa sekta binafsi ili kuongeza tija zaidi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akisalimia na Mwenyekiti na Rais wa Chemba ya Biashara na Viwanda ya Vietnam (VCCI) Bw. Pham Tan Cong walipokutana kwa mazungumzo jijini Hanoi, Vietnam.
Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo hayo umeongozwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Kombo.
Katika mkutano huo Wafanyabiashara wa pande zote mbili wamepata nafasi ya kushirikishana uzoefu wao na fursa za biashara na uwekezaji zilizopo na kupanga mikakati ya pamoja ya namna ya kutumia fursa hizo kwa manufaa ya pande zote mbili.
Miongoni mwa fursa zilizopata mwitikio mkubwa zaidi miongoni mwa wafanyabishara hao ni pamoja na zao la mkonge, vifaa vya ujenzi, uchumi wa buluu, madini hadimu, korosho na uwekezaji katika sekta ya kilimo.
Akizungumza katika mkutano huo Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bw. Vicent Minja amezisisitiza sekta binafsi kuchangamkia fursa zilizopo na zitakazo ibuliwa kwa manufa ya pande zote mbili.
Aliongeza kusema kuwa Serikali za pande zote mbili zimeonyesha utayari kwa kutengeneza mazingira mazuri ya biashara na zimekuwa zikitoa ushirikiano mzuri kwa wafanyabiashara hivyo ni vyema sekta binafsi ikatumia fursa hiyo kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kibiashara miongoni mwao ili kufikia malengo yanayokusudiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti na Rais wa Chemba ya Biashara na Viwanda ya Vietnam (VCCI) Bw. Pham Tan Cong ambaye pia alikuwa akiongoza ujumbe wa wafanyabiashara kutoka sekta mbalimbali, ameeleza utayari na shauku walioyonayo kufanya biashara na kuwekeza nchini Tanzania.
Aidha, ametoa rai kwa pande zote mbili kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa hapo awali, ikiwemo utekelezaji hati za makubaliano ya ushirikiano zilikwisha sainiwa.
Vilevile, Bw. Pham Tan Cong amependekeza kuanzishwa kwa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Vietnam litakalowawezesha wafanyabiashara kuongeza ushirikiano na uhusiano, pia kujadili na kushirikishana masuala mbalimbali ilikuongeza kasi ya biashara na uwekezaji kati ya pande hizo mbili.
Kwa upande wake Waziri Kombo amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi imara wa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango na nafasi ya sekta binafsi kwenye maendeleo ya Taifa hivyo itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa sekta binafsi ili kuongeza tija zaidi.
No comments:
Post a Comment