Habari za Punde

Jamii Yatakiwa Kujiimarisha Kwenye Kipato na Afya ya Akili.

Na. Mwanandishi  Wizara ya Afya.

Jamii imetakiwa kabla ya kufanya maamuzi ya kuongeza Mke wa pili wanatakiwa kujiimarisha kwenye kipato na afya ya akili.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt,Salim Slim katika ya Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Sayansi na elimu ya afya mbweni.

Amesema matatizo mengi ya afya ya akili yanatokana na baba kufanya maamuzi bila kujiweka sawa kiuchumi jambo linapelekea familia kupata tatizo la afya ya akili kwa kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya na mimba za mapema.

Nae mratibu wa kitengo cha afya ya akili Hamida Noufal Kassim amesema kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika mwaka 2023 zimeonyesha kuwa idadi kubwa ya wanaoathirika na tatizo la afya ya akili ni wananume.

Amesema wanaume wanatakiwa kujenga utamaduni wa kuzungumza na wanaowaamini juu ya matatizo yao yanayowakabili ili kujiepusha na matatizo ya afya ya akili.

Kwa upande wake mwakilishi wa haukeland university hospital AMALIA amesema wamekuwa wakishirikiana na kitengo cha afya ya akili kidongo chekundu katika kutoa huduma za afya ya akili unguja na pemba.

Nae meneja miradi kutoka HIPZ Dr.Juma Adnan Juma amesema wataendelea kushirikiana na wizara ya afya kwa kuendelea kutoa huduma ya upimaji wa afya ya akili kwenye jamii.

Amesema kuwa wanatarajia kuanza kutoa elimu ya afya ya akili kwenye sehemu za kazi ili kupunguza idadi ya wafanyakazi wanaosumbuliwa na matatizo ya afya ya akili.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani limesema Zaidi ya watu bilioni moja wanaishi na magonjwa ya afya ya akili duniani,ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni upatikanaji wa huduma za afya ya akili wakati wa majanga na dharura.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.