Habari za Punde

Ufunguzi wa Mafunzo ya Mawakala wa Vyama vya Siasa Wilaya ya Kaskazini " A" katika Skuli ya Gamba

Tume ya Uchaguzi Zanzibar  imewataka Mawakala wa Vyama siasa kuwa vyanzo vya utulivu wakati wa zoezi la upigaji kura.

kauli hiyo iliyolewa na Mjumbe wa Tume hiyo Mhe. Juma Haji Ussi wakati akifungua mafunzo ya Mawakala wa Vyama vya Siasa Wilaya ya Kaskazini " A" katika Skuli ya Gamba tarehe 11Oktoba, 2025,

Mhe. Juma alisema, Mawakala wa Vyama vya Siasa kimsingi wana nafasi kubwa ya kulifanya zoezi la upigaji kura kufanya katika hali ya amani na utulivu.

Mhe. Juma alisema, Mawakala ni vyema kushauriana na watendaji wa Tume vituoni kwa jambo lolote litakalotokezea kuliko kutawaliwa na mihemko ya kisiasa.

Hata hivyo, alithibitisha kuwa, kauli mbiu ya Uchaguzi Mkuu 2025 Zanzibar inatosha kusisitiza amani na ni vyema kutumika hadi katika vituo vya kupigia kura.

Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini "A" Miza Pandu Ali aliwaomba Mawakala wa vyama vya siasa kuzingatia maelekezo waliyopatuwa katika mafunzo na.kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi na wanachama wa vyama vyao.

Wakiwasilisha mada katika Mafunzo watendaji wa Tume Wilaya walisema kuwa, Tume ya Uchaguzi inaamini kuwa maelekezo waliyotolewa yatawawezesha mawakala wa upigaji kura, kuhesabu na kujumlisha kura kutekeleza majukumu yao kwa usahihi na ufanisi kituoni. 

walisema, Tume inaamini pia kuwa, Wakala wa upigaji, kuhesabu na kujumlisha kuwa watazingatia  maelekezo ya Sheria na kanuni za uchaguzi na wataheshimu utaratibu na wasimamizi wa kituo cha kupigia kura.

Nao Mawakala wa vyama vya siasa walithibitisha kuheshime maelekezo waliyopatiwa na viongozi wa Tume ya Uchaguzi na watendaji wake.




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.