Habari za Punde

Wahudumu wa Afya Jamii Kutumia Vyema Fursa ya Mafunzo Waliyoyapata Ili Kuwa na Mabadiliko Katika Jamii

Mkurugenzi  wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Shaib Ibrahim Muhamed  amewataka wahudumu ya afya jamii kuitumia vyema fursa ya mafunzo waliyoipata ili kuwa na  mabadiliko Nyanja katika jamii.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kufunga mafunzo ya stadi ya maisha kwa Wahudumu wa Afya Jamii (CHW) 50, kutoka Shehia mbali mbali za Unguja katika Ukumbi wa Kituo cha Mafunzo ya Vijana Bweleo, Wilaya ya Magharibi ‘B’.

Amesema lengo la  mafunzo hayo ni kuwapa nguvu vijana waelimishaji rika katika harakati za kuelimisha jamii jambo mbalo litasaidia kuleta mafanikio na kufikia lengo la mradi huo.

Aidha amewataka wahudumu hao kuhakikisha taaluma hiyo inafika katika jamii na mafunzo hayo kuwa endelevu jambo ambalo litasaidia  kubadilisha tabia kwa vijana.

Alifahamisha kwamba vijana wanamahitaji mengi ili kufikia katika mazingira bora hivyo elimu ya stadi za maisha inahitajika kwa kuweza kuwasaidia kufikia maamuzi sahihi ya malengo yao.

Hata hivyo aliwaasa wahudumu hao kudumisha Amani na utulivu wa nchi katika kipindi hichi cha  Kampeni kuelekea Uchaguzi  Mkuu 2025.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wahudumu wenziwe  Bi Asia Fadhil Makame kutoka Shehia ya Mkokotoni ameishukuru Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana kwa kutoa mafunzo hayo na kuahidi watayafanyia kazi kwa ufanisi.





Imetolewa na Kitengo cha Habari,WHVUM.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.