Habari za Punde

WABUNGE KUTOKA ZANZIBAR WATEULIWA MAWAZIRI NA MANAIBU NA RAIS KIKWETE

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo hii ametangaza baraza lake la Mawaziri ambalo litakuwa na wizara 29.

Wizara za Mambo ya ndani ya nchi, Ulinzi, pamoja na Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia zimeangukia kwa Wabunge kutoka Zanzibar.

Miongoni mwa waliobahatika kuteuliwa kushika nafasi za Waziri na Naibu Waziri kutoka Zanzibar ni wafuatao.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi - Shamsi Vuai Nahodha

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi

Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi ya Teknolojia - Profesa Makame Mnyaa Mbarawa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Waziri anayeshughulikia Muungano - Samia Suluhu Hassan

Naibu Waziri Wa Fedha (Ina Manaibu wawili wa fedha) - Pereira Silima

Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki - Abdallah Juma Abdallah

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa - Mahadhi Juma Maalim

 
Miongoni mwa Mawaziri waliokuwemo katika Baraza la Mawaziri lililopita na ambao hawakubahatika kurudi ni Dr Maua Daftari, Mohammed Seif Khatib, Mohammed Aboud, Omar Yussuf Mzee, Balozi Idd Seif.

Ni Waziri wa Ulinzi pekee Dr Hussein Mwinyi aliebahatika kurudi katika nafasi yake. Balozi Idd Seif ni Makamu wa pili wa Rais katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Omar Yussuf ni Waziri wa Fedha wa Zanzibar na Mohamed Aboud ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Uteuzi wa Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kuongoza Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia umeleta baadhi ya masuala kwa baadhi ya wananchi wakidai Wizara hii si ya Muungano na kwa hivyo haipaswi kupewa Mbunge kutoka Zanzibar.

Blog yako inawapa hongea walioteuliwa na kutarajia watatekeleza wajibu wao kwa kuhakikisha maslahi ya Zanzibar katika Muungano yanasimamiwa vyema.

5 comments:

  1. Mbona Mahadhi Juma Mahadhi umemuacha? Naibu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

    ReplyDelete
  2. Tumerekebisha Mdau. Shukran kwa angalizo

    ReplyDelete
  3. Mahadhi Juma Maalim sio Mahadhi Juma MAHADHI

    ReplyDelete
  4. Sawa mkuu tumesahihisha. Ahsanteni sana wadau hasa kwa kututanabahisha na makosa ya kiuandishi.

    ReplyDelete
  5. waziri wa ulizi si mzanzibar Dr Hussen mwinyi hata baba yake tulipompa urais wa zanzibar hakujuwa kama alitawala nchi inayoitwa zanzibar hata Hussen mwinyi tulipoletewa jina lake kwenye baraza letu tukufu tulisema huyu si mzanzibar hawezi kuwa RAIS WA ZANZIBAR TULIFANYA MAKOSA KUMBA BABA YAKE URAIS AMBAO HAJUI HADHI YAKE TULISHASEMA ZANZIBAR ITAJENGWA NA WAZANZIBARI WENYEWE

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.