Vinavyohitajika
Ukwaju 100g
Sukari 200g lakini utaangalia kiasi ukipendacho
Arki ya portessa flavour kijiko 1 cha chai (arki hii ni maarufu inapatikana Afrika)
Nanasi kama likiwa dogo 1 au nusu kama kubwa
Namna ya kutayarisha na kutengeneza
Roweka ukwaju na sukari kwa maji ya moto na uwache kwa nusu saa.
Menya nanasi na ulisage kwenye blender ili upate juice.
Weka pembeni juice ya nanasi.
Saga ukwaju kwenye blender pamoja na sukari uliyoiroweka.
Ichuje juice hiyo ya ukwaju na nanasi.
Changanya juice hizo mbili na umalizie kwa kuweka arki.
Koroga vizuri na weka barafu na tayari kwa kunywewa.
Kidokezo
Unaweza kuigandisha ikawa barafu na ukaiblender ikawa kama smoothy (zito zito), pia unaweza kufanya juice hii ya ukwaju kwa kuchanganya na tunda la peach inakuwa na ladha nzuri.
RAIS SAMIA ATOA NENO KWA DKT. MWIGULU DHIDI YA VISHAWISHI VYA MARAFIKI WA
MADARAKA
-
Na Janeth Raphael - MichuziTv -Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtakia
kheri Waziri Mkuu mpya wa Tanzania Dkt...
1 hour ago


safi sana asante kaka. Ndio nipo mbioni kujaribu kutengeneza
ReplyDeleteThankx
ReplyDelete