Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya leo, Jumamosi, Septemba 10, 2011, ametembelea Viwanja vya Maisara mjini Zanzibar kujionea mwenyewe zoezi la kutambua miili iliyoopolewa kutoka baharini kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander alfajiri ya kuamkia leo.
Akifuatana na Mama Salma Kikwete, Mheshimiwa Rais Kikwete amewasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar saa 12:10 jioni na kwenda moja kwa moja kwenye Viwanja vya Maisara ambako mamia kwa mamia ya waombolezaji walikuwa wamekusanyika kujaribu kutambua miili za jamaa, ndugu na wapendwa wao ambao wamepoteza maisha katika ajali hiyo.
Kwenye Viwanja hivyo, Rais Kikwete amepokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ) Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wawili wa Rais wa Zanzibar, Waheshimiwa Seif Sharif Hamad na Balozi Seif Idd, Rais Mstaafu wa Zanzibar Mheshimiwa Amani Abeid Karume na uongozi karibu wote wa juu wa SMZ.
Hali ilikuwa ya huzuni sana kwenye Viwanja hivyo wakati Mheshimiwa Rais akifuatana na uongozi huo wa juu wa Zanzibar ulivyopitia kwenye mahema ya muda ya zoezi ya utambuzi wa miili ya watu waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo ya meli hiyo iliyokuwa inasafiri kutoka Dar-Zanzibar-Pemba. Imezama katika eneo la Nungwi, Zanzibar.
Katika eneo hilo la utambuzi, Mheshimiwa Rais ameshuhudia miili ya watu wazima iliyokuwa imefungwa ama kufunikwa na ile ya watoto wadogo ambao sura zao zilikuwa zimeachwa wazi kwa ajili ya utambuzi wa haraka kwa mujibu wa sura zao.
Kwenye Viwanja hivyo, Mheshimiwa Rais ameambiwa kuwa hadi jioni hiyo ya leo, watu kiasi cha 192 walikuwa wamethibitishwa kuwa wamepoteza maisha na miili yao kuopolewa wakati kiasi cha watu 630 walikuwa wameokolewa kutoka ajali hiyo ya meli ambayo hadi sasa haijulikani ilikuwa imebeba watu wangapi.
Baadaye, Rais Kikwete ametembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwaona na kuwatakia heri waliokoka katika ajali hiyo na kulazwa katika hospitali hiyo ya Serikali.
Hadi jioni ya leo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilikuwa imechukua maamuzi kadhaa kukabiliana na hali ya ukoaji wa watu katika ajali hiyo. Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kuchangia kiasi cha sh milioni 300 ili kusaidia zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kusaidia kusafirisha na kuzika miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo. SMZ imetoa sh milioni 100 kwa shughuli hiyo.
Serikali ya Muungano pia imeamua kukubali msaada wa wapigaji mbizi kutoka Afrika Kusini kwa ajili ya kusaidia kufanya tathmini ya jinsi meli ilivyozama na kuokoa maisha ya watu ambao watakuwa wamebanwa ndani ya meli hiyo.
Kesho, Jumapili, Septemba 11, 2011, Kamati ya Taifa ya Ulinzi na Usalama itafanya kikao chake mjini Zanzibar kuzungumzia hali ya ajali hiyo kwa maana ya kupata maelekezo kamili kuhusu ajali hiyo, kupokea ripoti ya ajali, kufanya tathmini ya ripoti hiyo na kutoa maelekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali ya sasa na hali ya baadaye ya usafiri wa maji nchini.
Hata kabla ya kikao hicho, tayari Mheshimiwa Rais Kikwete ameamua kufanyika kwa uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha ajili hiyo.
Labels
- .
- `
- 8
- AFYA
- AFYA.
- AJALI
- BIASHARA
- BURUDANI
- DINI
- ELIMU
- FILAMU
- HABARI
- HARUSI
- HOSPITALI
- I
- JAMII
- KATUNI
- Kii
- KILIMO
- KIMATAIFA
- KITAIFA
- Ku
- MAGAZETI
- Mahkamani
- MAISHA
- MAKALA
- MAKALA AFYA.
- MAKALA.
- MATUKIO
- MATUKIO.
- MICHEZO
- MITAANI
- MIUNDOMBINU
- MSAADA
- Ok
- SIASA
- TANGAZO
- TAWA YAWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI
- TEKNOLOJIA
- UCHUMI
- UTAFITI
- UTALII
- VIDEO
- VIJANA
- VISA INTERNATIONAL YAZINDUA TAWI TANZANIANa Mwandishi wetu 16.07.2025DAR ES SALAAM
- WEZI
Tafsiri ya Lugha
Popular Posts
-
A K Simai Yalipotoka Matokeo ya kidato cha Nne ambayo yalikuwa mabaya kufikia baadhi ya Skuli za Zanzibar kufutiwa Mitihani pamoja na ku...
-
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ( wan ne kutoka kulia) akikagua vifaa vitakavyotumika katika mradi wa njia ya ...
-
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mhe.Jaji Goerge Joseph Kazi akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vyeti vya Uteuzi wa Wagom...
-
Mama mjazito akihangaika na hatimaye kupoteza maisha kutokana na mimba za utotoni..Video ipo hapo chini baada ya maelezo mafupi
-
Bwana Harusi Lusajo Sajent Mwangambaku (kushoto), akiwa katika pozi na mke wake Neema Stanley Matowe katika hafla yake ya ndoa iliyofa...
-
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ambae ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni R...
-
Na Miza Kona/Rahma Khamis Maelezo-Zanzibar Jumla ya wanafunzi 16,744 wamechaguliwa kuendelea masomo ya kidatu cha tatu kati ya wanafun...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
BLOGU RAFIKI
-
-
KAMATI UTEKELEZAJI MKAKATI WA MUDA WA KATI WA MAPATO MIAKA 3 WAZINDULIWA DODOMA. - Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt Natu Mwamba amesema kuwa lengo kuu la Mkakati wa muda wa kati wa Mapato ni pamoja na...42 minutes ago
-
Elimu : Awamu ya Sita Yaipiga Jeki Elimu, Walimu Wapongezwa Arusha - Na Pamela Mollel, Arusha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya maboresho makubwa katika sekta ya elimu mkoani Aru...12 hours ago
-
MAHOJIANO YA TAUSI SUEDI NA AMRI NGOYE KUHUSU CSI KUPITIA KWANZA PRODUCTION NCHINI MAREKANI - Pata habari motomoto kupitia facebook kwa kulike huu ukurasa wetu https://www.facebook.com/pages/Pamojapureblogspotcom/312633955485619?ref=hl7 years ago
Marafiki Duniani
Popular Posts
-
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili Zanzibar majira ya mchana kwa Ndege na kuendelea na taratibu za Maziko yatafanyika katika Mtaa wa...
-
The United Republic Of Tanzania National Examination Council of Tanzania Form Four Examination Results 2017/2018 The National E...
-
Makamanda wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Waziri Kiongozi wa Kwanza wa Zanzibar na Brigedia Jenerali Mstaaf Ramadhani Haji Faki...
-
Na Miza Kona/Rahma Khamis Maelezo-Zanzibar Jumla ya wanafunzi 16,744 wamechaguliwa kuendelea masomo ya kidatu cha tatu kati ya wanafun...
-
Bwana Harusi Lusajo Sajent Mwangambaku (kushoto), akiwa katika pozi na mke wake Neema Stanley Matowe katika hafla yake ya ndoa iliyofa...
-
Mama mjazito akihangaika na hatimaye kupoteza maisha kutokana na mimba za utotoni..Video ipo hapo chini baada ya maelezo mafupi
-
Hutuba ya Mhe Waziri wa Afya Nd. Mahmoud Thabit Kombo kwa Waandishi wa Habari Katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Dunia Zanzibar, 22...
-
Madawa na Maji vilivyokabidhiwa na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya Kambi za K...
No comments:
Post a Comment