Habari za Punde

KUTOKA BARAZANI - MAZRUI ASTOPISHA UUZWAJI VIWANDA VYA SERIKALI

WIZARA ya Biashara, Viwanda na Masoko, imesema kuanzia sasa hakuna kiwanda chchote cha serikali kitachouzwa na badala yake itavifanyia uhakiki na kuvisajili viweze kutambulika.

Waziri wa Wizara hiyo, Nassor Ahmed Mazrui, aliyasema hayo jana wakati akijibu suali la Mwakilishi wa Matemwe, Abdi Mosi Kombo, aliyetaka kujua kama serikali ina mpango wa kuvifufua na kuvirudisha viwanda ili wananchi waweze kupata ajira.


Akijibu hoja hiyo Waziri huyo alisema serikali katika utekelezaji wa sera ya kulinda viwanda hivi sasa haina mpango wowote wa kuuza viwanda viliopo na imo katika mpango wa kuvihakiki mali za viwanda vyote viliomo chini ya usimamizi wa serikali.

Alisema ni kweli hapo awali sekta ya viwanda ilisaidia kuwapatia ajira wananchi wengi wa Zanzibar, lakini kutokana na serikali kujiondoa katika biashara imelazimika kuachia viwanda hivyo ikiwa ni hatua ya kufungua milango zaidi kwa Wawekezaji.

Alisema kutokana na uamuzi wake huo, serikali iliamua kuviuza viwanda vyake vingi na vichache ilibaki navyo ambapo kati ya viwanda ilivyoviuza ni pamoja na cha Sabuni na mafuta ya nazi.

“Serikali itaendelea kujikita katika uwekaji wa mazingira bora kwaajili ya uwekezaji wa miradi ya sekta binafsi, ikiwemo miradi ya viwanda au kufufua viwanda vya zamani” alisema Waziri huyo.

1 comment:

  1. Yale...yalee! kuuliza swali ilimradi tuu! Hebu jamani tuweni 'realistics' kidogo. Tatizo la ajira hapa linaweza kumalizwa na sekta 2 tuu:- utalii na uvuvi kama zikisimamiwa vyema.
    Utalii; SMZ kupitia W/elimu iwajenge vijana kisaikolojia waamini utalii ni kazi kama ulivyo 'ualimu' udaktari uwanasheria n.k. Wenzetu Kenya na T/Bara kijana wa DV.(11) FORM 6 unakuta anasoma 'H/management' AU 'food production' ndani au nje ya nchi, badae nakuja ZNZ kua H/manager au chef mahali analipwa ml. 3 au 4 ..sie twaonewa!..eti viwanda kwenye soko la watu ml.1200,000?
    Uvuvi; hii sekta pia inaweza 'kututoa' tuna bahari ya kutosha,samaki wengi,soko la uhakika(hasa la ndani)..manake kula samaki ZNZ inaelekea kua 'anasa' labda dagaa na tuna vijana wengi wenye uzoefu hasa kule Nungwi, Kojani nk. ni suala la kujipanga tu na kutafuta uwekezaji. Lkn. hapa sio viwanda wala kilimo..maana ardhi haitoshi labda mboga mboga! tutumieni'Principal of comparative advantage' tusomesheni vijana KISWAHILI vizuri waende nje wakawe waalimu, wakalimani na watangazaji kwa vile bado watu wanaamini sisi tunakijua vizuri!..tuacheni ndoto za mchana SMZ haitaweza kuajiri vijana wote hao! mtalaumu bure na kuonea serikali!...hapo vp?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.