Habari za Punde

TAMASHA LA EPIQ NATION VIWANJA VYA KISONGE LAFANA.

 Wananchi wakiwa katika Viwanja vya Kisonge  Michezani wakifuatilia  Tamasha la Apiq, likiburudishwa na Wasanii kutoka Dar-es- Salaam wakitowa burudani jana usiku.
 Hivi ndivyo ilivyokuwa Viwanja vya Kisonge Michezani Zanzibar.
MC akitowa vionjo kwa Wapanzi wa Muziki wa Bongo Flava, ikiwa ni Tamasha la Epiq Nation.la Kampuni ya Simu za Mikononi ZANTEL.  
Wapenzi wa muziki wa Bongo Flava  wakiwa katika viwanja vya Kisonge Michezani wakisubiri kuanza kwa Tamasha hilo ambalo limeaza saa 12.00 jioni hadi saa tatu usiku,  
 Msanii wa Bongo Flava Mr Blue akitowa burudani katika viwanja vya Kisonge Micjezani.
 Wapenzi  wa muziki wa Bongo Flava wakimsherehekea msanii Mr Blue alipokuwa jukwaani.
Msanii Matonya akifanya vitu vyake katika jukwaa wakati wa  Tamasha la Epiq Nation katika viwanja vya Kisonge Michezani, akitowa  mistari yake. 
DJ. akifanya vitu vyake akipanga ngoma katika tamasha hilo. 
 Msanii Sharobaro Orijino akilishambulia jukwaa katika onesho la Tamasha la Epiq Nation lililofanyika viwanja vya Kisonge Michenzani.







 Msanii A T, akiimba wimbo wake wa Samaki.  
Mambo ya mduwara wakati wa alipopanda jukwaani Msanii AT, ameshinda kujizuiya sehemu yake na kuaza kuyarudi.   

4 comments:

  1. I hope watoto hawakuwepo wakati wa mduara huu. Ama kweli watanganyika hawatatuachia mpaka tufuate mila zao. Allah hakukosea kwa hili aliposema kwenye aya ya 120 suratil Baqara. Kuwa hawataridhia mayahudi na wakristo mpaka mufuate mila zao. Matamasha haya kutoka Tanganyika hayana lengo jengine isipokuwa ni kututoa wanzibari katika mila zetu na kuwafanya watoto wetu na vijana wetu wasipende utamaduni wao asili baadae waige uvaaji wa suruali wa hao waimbaji, mikato yao ya nywele na mengineyo. Sijui lini tutaamka wazanzibari.

    ReplyDelete
  2. Ujumbe mzuri lkn. umezidiwa na ushabik! Hivi tujiulize, wamekuja wenyewe ua wameletwa na z'tel? na huu mtandao ni wakinanani? Mm nadhani tunapolaumu, busara zitawale.Kama kweli hatutaki matamasha ya namna hii, basi ofisi za Z'tel hazipo mbali!

    ReplyDelete
  3. Mimi labda niulize kwani hakuna sehemu nyengine ya kufanyia matamasha haya ziadi ya Kisonge? Imagine zogo kama hili na sehemu ile imezungukwa na nyumba humo kuna wengine watu wazima, wengine wagonjwa na kadhalika.

    Nadhani Manispaa waliangalie hili eneo kwa matamasha ya aina hii nadhani si muwafaka

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.