Habari za Punde

Warsha ya Ongezeko la Uvuvi Haramu na Hasara zake katika Visiwa vya Zanzibar.


Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho, akifunguwa Warsha ya siku moja juu ya Uvuvi harama unaotumiwa na baadhi ya Wavuvi Unguja na Pemba, iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Zanzibar Said Ali Mbarouk, akitowa maelezo machache kuhusi mafanikio ya Wizara yake kupambqana na Uvuvi haramu, wakati wa Ufunguzi wa Warshi hiyo huko Hoteli ya  Zanzibar Beach Mazizini.  
Naibu Katibu Mkuu Wizaya ua Mifugo na Uvuvi Dk.Omar Ali Amir, akizungumza katika warsha hiyo.  wanaotoa bletowa  
Baadhi ya washiriki wa Warsha ya Ogezeko la Uvuvi haramu, wakimsikiliza Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, akifunguwa semina hiyo ilioandaliwa na Idara ya Kuendeleza Uvuvi Zanzibar, na kuwashirikisha Viongozi wa Siasa, Wavuvi na Masheha. kuzungumzia athari za uvuvi haramu wa kutumia Nyavu za Macho madogo Uvuvi wa bunduki na wa kutumia baruti.    
Viongozi wa meza kuu wakimsikilza Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Zanzibar Mussa Aboud Jumbe, akitowa maelezo ya Uvuvi haramu, katika warsha ya kutowa elimu kwa Wavuvi jinsi ya uvuvi unaofaa na kutunza mazingira ya bahari na mazalio ya samaki baharini. 
Viongozi wa Serikali na Vyama wakimsikiliza Spika wa Baraza la Wawakilishi akifunguwa semina hiyo iliofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini Unguja.
Waandishi wa habari wakiwa makini kuchukua habari katika semina ya kuelimisha uvuvi haramu unaofanywa na baadhi ya wavuvi wanapokuwa baharini.  
Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Zanzibar Mussa Aboud Jumbe, akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada ya uvuvi  haramu na vifaa wanavyotumia wavuvi, wakiwa katika kazi zao za uvuvi ambazo zimepigwa marufuku kutumia kwa mujibu wa sheria ya uvuvi ya mwaka 2010 iliopitishwa na Baraza la Wawakilishi.  
Mkurugenzi wa Uvuvi Zanzibar Mussa Aboud Jumbe, akiwaonesha washiriki wa semina hiyo baadhi ya Nyavu za macho madogo walizozikamata katika bahari ya Unguja, ambazo hasiruhusiwi kutumika katika uvuvi kwa sababu huvua samaki wadogo. 
Viongozi wa meza kuu wakifuatilia mada ya Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Zanzibar Mussa Aboud Jumbe, alipokuwa akitowa mada yake kuhusu utumiaji wa vifaa vya uvuvi visivyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya Uvuvi Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Mussa Aboud Jumbe, akionesha dema walilolikamata ambnali lina macho madogo, kinyume na sheria za uvuvi.wakati wa semina hiyo iliofanyika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.   
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano wa uvuvi haramu.


Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Mussa Aboud Jumbe, akionesha dema walilolikamata ambnali lina macho madogo, kinyume na sheria za uvuvi.wakati wa semina hiyo iliofanyika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.
Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Zanzibar Mussa Aboud Jumbe, akionesha moja ya nyavu haramu walizozikamata wakitumia wavuvi baharini kuvyulia samaki,Mdau hii siyo nyavu bali ni chandarua kimeshona na kutumia kufulia samaki.
Mwakilishi wa Kitope Makame Mshimba, akichangiya katika semina hiyo ya kujadili uvuvi haramu unaofanywa na baadhi ya wavuvi kukiuka sheria iliowekwa ya kutotumia vifaa visivyofaa kufulia samaki.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Wavuvi wa Kojani (KOFDO) amesema wao huzingatia uvuvi halali ulioruhusiwa na Idara ya Uvuvi na kutumia vifaa halali kwa uvuvi wao na sio kuona wakiwa wengi katika boti basi huvua uvuvi haramu. wanatii sheria hiyo na kutowa elimu kwa wanachama wao wakojani jinsi ya uvuvi halali unaotakiwa kutunza mazingira ya barahi na kuhifadhi mazalio ya samaki.   
Mdau Vyama vya Siasa kutoka CUF Masoud Khamis,amesema wakati wa miaka ya nyuma wavuvi hawauzi samaki wao bila ya kukaguliwa na kupasisha ndio wauze, inahitajika kutumiwa sheria hiyo ya wakati huo amesema Waziri wa Uvuvi alikuwa Ibrahim Makungu, Pia amempongeza Mkurugenzi wa Uvuvi kwa kufuata sheria na kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria lakini wavuvi ndio wanaovunja sheria hiyo na kutumia vifaa haramu vya kuvulia.  
Mdau wa jenda nae hakuwa nyma ilibidi na yeye kuchangia mada ya uvuvi haramu
Mwandishi wa ZBC Redio Said Suleiman, ameipongeza Idara ya Uvuvi kwa kuwaalika waandishi katika semina hiyo ya kuzungumzia uvuvi haramu waandishi ndio chombo cha kuelimisha jamii na kutowa taaluma kwa Wananchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.