Habari za Punde

Eco, PIC Zatiliana Saini Kuimarisha Uchumi

Joseph Ngilisho, Arusha

BENKI ya Eco kwa kushirikiana na shirika la uwekezaji wa sekta ya umma la Afrika ya Kusini(PIC) imetia saini mkataba wa dola za Kimarekani Milioni 250 kwa ajili ya kukuza na kuimarisha shuguli mbalimbali za Miradi ndani ya nchi za bara la Afrika.

Akizungumza mara baada ya kutiliana saini mkataba huo, Mkurugenzi wa Eco Benki, Anolrd Ekpe, alisema kuwa kuanzia sasa zoezi la kuimarisha miradi mbalimbali kwa nchi za bara la Afrika zinaanza rasmi.

Alifafanua kuwa mpango huo ambao unaanza kwa nchi za bara la Afrika utakuwa na nafasi kubwa ya kuruhusu uwekezaji wa hali ya juu, ambapo hata benki hiyo inaweza kuimarisha uchumi.

Pia alisema kupitia makubaliano hayo baina ya benki hiyo na PIC, pia kutaweza kuongezeka kwa shughuli mbalimbali za uwekazaji katika bara la Afrika hali ambayo itachangia kukua kwa uchumi ambapo ndilo lengo halisi la makubaliano hayo.

“Huu mpango ambao utaenda kwenye nchi 32 za bara la Afrika zitaweza kutumia vyema mkataba huo ambapo kupitia hata mpango huo uchumi nao utaaimarika sana na hata kiwango cha uwekezaji nacho kitapanda tofauti na sasa ndani ya nchi hizo”aliongeza Bw Anorld

Awali alifafanua kuwa kupitia mchakato huo wa nchi 32 za bara la Afrika nayo Eco Benki itaweza kunufaika sana kwa kuwa mapato yake nayo yataweza kuongezeka kwa kiwango cha asilimia 19.58 hali ambayo nayo ni nzuri kwa ajili ya shuguli mbalimbali za uwekezaji wa bara la Afrika.

Anorld alisema kuwa ili kuweza kuimarisha hata uchumi wa nchi mbalimbali za bara la Afrika wamejiwekea Mikakati maalumu wa kuhakikisha kuwa kila jamii inafikiwa na huduma muhimu kwa ajili ya kukuza na kuimarisha uchumi ambao ndio lengo halisi la Benki hiyo.

Alitaja Mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa benki hiyo inajikita zaidi kwenye kila kona ya nchi ambapo kupitia kona hizo wataweza kuwekeza kwa kiwango cha hali ya juu, jambo ambalo liatachangia kuimarika kwa uchumi barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.